| Mike Sangu na Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ siku ya ndoa yao. | 
Chanzo cha habari hii ambacho ni rafiki wa Thea kilieleza kuwa, 
kutibuana kwa wanandoa hao kumekua kufuatia Thea kuhisi mwenzake 
anamzunguka.“Kimsingi hali si shwari, ndoa inawaka moto, Thea anamtuhumu
 Mike kuwa anamsaliti, chanzo ni hizi simu na siku hiyo mtiti 
ulipotokea, shosti alikwenda kwao na mpaka leo hii (Juzi Jumatato) 
anasubiri wasuluhishwe,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo, Mike alitafutwa na alipoulizwa kuhusu 
ndoa yake kutibuka alisema: “Mh! Watu ni wambeya sana mimi na mke wangu 
tulitokea kutoelewana na si mambo ya meseji wala wanawake, mimi sina 
mambo hayo kabisa, siwezi kuongelea mambo mengi mpaka nitakapoenda 
nyumbani kwa mke wangu lakini kilichotokea ni cha kawaida tu .”Thea 
hakuweza kupatika kuzungumzia ishu hiyo.



0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....