Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma,Deusdedit Nsimek akionyesha nyara za serikali (mikia ya tembo) zilizokamatwa na Jeshi la Polisi MKoani humo.Nyara za Serikali ambazo zimekamatwa(mikia kumi ya tembo)
Na Demasho Blog.
Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma linamshikiria kijana ambaye anafahamika kwa jina la Bakari Said mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mkazi wa eneo la Mbalikiwa kata ya Ligunga Wilayani Tunduru kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali (mikia ya tembo).
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma,Deusidedit Nsimeki ameyasema hayo leo mapema wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema jumla ya mikia ya Tembo 10 imekamatwa na askari ambao walikuwa doria katika eneo la Mbalikiwa mnamo tarehe Aprili 5, 2013 majira ya saa:7 usiku ambapo jumla ya idadi hiyo ya mikia ni sawa na idadi ya Tembo 10 waliouwawa na idadi ya meno ni 20 yenye jumla ya dola za kimarekani elfu 15 sawa na zaidi ya milioni 245 kwa fedha za kitanzania.
Mtuhumiwa Bakari Said leo alifikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara hiyo haramu ya nyara za serikali ambapo taharifa ya tukio hilo la uhalifu zilipatikana kutoka kwa raia wema pia kamanda wa polisi aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wao wa dhati ili kuweza kudhibiti kabisa huarifu huo.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....