LINAH, AMINI WAFUNGUA UKURASA MPYA WA PENZI LAO....!!



ESTELINA Sanga ‘Linah’ na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Amini Mwinyimkuu wamenaswa katika pozi jipya la kimahaba zaidi.
Picha hiyo inayowaonesha wawili hao wakiwa ndani ya gari huku mwanadafada akimbusu Amini, imedakwa juzikati katika mtandao wa BBM, ambapo wadau wanaotumia mtandao huo waliwapongeza kwa kurudiana.

Chanzo chetu kilimtafuta Linah, alipopatikana alijibu kwa kifupi kwamba hana tatizo na Amini hivyo yupo huru kwa lolote mbele yake na wanafanya naye kazi kwa karibu.
Kwa upande wake Amini,  alipoulizwa juu ya ishu hiyo alitiririka: “Linah ni mtu wangu hivyo sina ubaya naye kwa kila kitu hatujawahi kugombana wala kusutana picha zisiwashtue watu,” alisema Amini.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter