DEREVA anayetuhumiwa kwa kesi ya kusababisha kifo cha askari wa usalama barabarani, Koplo Elikiza Nnko, Jackson Steven Simbo (pichani) amefikishwa mahakama ya Kinondoni, Dar, Machi 26, mwaka huu na kuzua jambo kortini.
Mtuhumiwa huyo baada ya kupata dhamana alikwenda ofisini kwa maofisa wa mahakama hiyo na kubadili shati kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuondoa nuksi ya kulala rumande kwa siku 8.
Jackson anakabiliwa na makosa matatu, kusababisha kifo cha Koplo Elikiza, kuendesha gari kwa mwendo kasi na kuingilia msafara wa kiongozi na kushindwa kujisalimisha polisi hadi alipokamatwa. Kesi hiyo itatajwa tena Aprili 15, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....