Tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita lilimfanya Wema kuinuka na kupangusa makalio yake kisha kushika hamsini zake akiwaacha wasanii wengine waliokuwa katika kikao hicho wakipigwa na bumbuwazi.
Gazeti la Amani baada ya kuzinyaka taarifa hizo lilimsaka Wema na kumuuliza kulikoni alikimbie neno skendo, naye alikuwa na haya ya kujibu:
“Nani asiyejua kama ninaandikwa sana kwa skendo kwenye magazeti? Sasa mtu anasimama mbele yangu, anatoa hoja kwa kusema ustaa siyo
kuwa na skendo, mbaya zaidi ananitolea macho, sasa unafikiri miye nitatafsiri vipi?” alihoji Wema.
Kama vile haitoshi malkia huyo wa filamu alisema kuwa mzungumzaji alijiandaa kumdhalilisha au alitumwa na watu ili afanye vile kwa makusudi.
“Sikutaka shali ndiyo maana nikaamua kutimua zangu kwa kuwa huwa sipendi ajenda zisizokuwa na kichwa wala miguu,” aliongeza.
Pia, Wema ambaye ni mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006 alisema mzungumzaji aliponda skendo kwa kuwa si staa na hajulikani, laiti angekuwa anajulikana asingeongea utumbo kama aliokuwa akiuongea.
“Huwezi kuwa staa bila ya kuandamwa na skendo na kila sehemu kuna aina yake ya skendo, kwa mfano siasa ina aina yake ya skendo na michezo halikadhalika, namshangaa yule mbwiga anayetafuta ustaa kupitia majina ya watu,” alisema kwa hasira
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....