PICHA: KIJANA AJINYONGA KUKWEPA AIBU YA KUFELI MTIHANI WA KIDATO CHA NNE AMBAO ANADAI KUWA ANAUHAKIKA ANGEFELI TENA...


Mwanafunzi  aliyekuwa akisubiri kufanya  mtihani  wa kidato cha nne unaotaraji  kuanza kesho Bw Khamis Mkundo mkazi  wa Mwangata C katika Manispaa  ya Iringa  akiwa amejinyonga  usiku  huu kuhofu  mtihani  wa kidato cha nne
 Mwenyekiti  wa serikali ya mtaa wa Mwangata C Bw Sarehe Mgimwa akisoma ujumbe  ulioachwa na marehemu huyu 
 Askari  kanzu  akikagua  mwili wa mwanafunzi  huyo  


 Wananchi  wa Mwangata  mjini Iringa  wakiwa nyumbani kwa marehemu  
 Mwili  wa kijana  huyo ukitolewa  tayari  kupelekwa  chumba  cha kuhifadhia maiti Hospital  ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa
Mwili  huo ukipakiwa katika gari  la  polisi


Mwanafunzi   aliyekuwa akisoma  shule  ya  sekondari  Sabasaba  mjini  Iringa akijiandaa kurudia  kufanya  mtihani  wa  taifa  wa kidato  cha nne kupitia  kituo  cha Krelluu mjini  Iringa Khamis Mkundo  mkazi  wa Mwangata  C katika manispaa ya  Iringa amejiua kwa kujinyonga  kwa kamba kwa kile  alichodai  kuchoshwa na kufeli  mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.

Katika  barua  yake  ndefu aliyoiandika  kijana  huyo amesema  kuwa amefanya  hivyo si kwa kujipendea  ila amechukizwa na hatua yake ya  kufeli mara kwa mara  hivyo  kuamua  kujiua ili  kuepuka na aibu katika mtihani ujao ambao anaamini angefeli.

Shemeji  wa  kijana  huyo Aden Tagalile ameueleza mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com  kuwa  tukio  hilo limetokea mida ya  kati ya saa 12 na saa 1  usiku wa  leo baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda  mrefu  kwa kijana  huyo kuonyesha kuchukia hatua yake ya kuendelea kuristi  mtihani  wa kidato cha nne  bila mafanikio.

Kwani  alisema hajapenda  kuona anaendelea  kufeli na kuwa  yupo tayari kwa lolote  kukwepa aibu ambayo ipo mbele  yake.

Hata  hivyo kufuatia mazungumzo hayo kijana huyo aliangana na ndugu zake akiwemo kaka  yake anayeishi nae kwa kila mmoja kuondoka nyumbani  hapo kabla  ya kijana  huyo kukutwa amejinyonga.

Mwenyekiti  wa serikali  ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha  kutokea kwa kifo  hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana  huyo ameuacha .

CHANZO: MATUKIO DAIMA

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter