HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYAKAZI NA WANAWAKE WAREMBO..!!

Kufanya kazi sehemu moja au kuzungumza na mwanamke mwenye mvuto kunaweza kumfanya mwanaume apoteze umakini wake, hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la New Study.

Wanaume wanaofanya kazi kwenye makampuni yenye ‘visura’ wengi, ufanisi wao ni wa kiwango cha chini kulinganisha na wasiokuwa kwenye mazingira hayo, sehemu ya utafiti inaeleza.
Sababu ya kuwepo kwa hali hiyo ni uchunguzi kubaini kuwa, akili za wanaume wenye kuvutwa na sura wakati wakifanya mambo hukabiliwa na mgongano wa hisia mbili, za kazi na mapenzi.
Kuwepo kwa vitu hivyo viwili kwa wakati mmoja ndani ya akili ya mwanaume, utafiti wa kitaalamu uliochapishwa na Jarida la Journal of Experimental and Social Psychology, umebaini kuwa mwanaume ana hatari kubwa ya kufanya vibaya kikazi kwa sababu wakati akifanya kazi yake atakuwa pia akifanya kazi ya kushawishi au kuimarisha hadhi yake mbele ya mwanamke aliyemvutia.
Ukichunguza, utabaini kuwa, tabia za wanaume (si wote) hubadilika pindi wanapokuwa mbele ya wanawake warembo, hii ikiwa na maana kuwa, kama mwanaume ni mwenye maneno mengi na mpayukaji kwa mfano, hujikuta akilazimika kushusha sauti yake, kuongea kwa unyeyekevu na busara lengo ni kutaka kumvutia msichana.
Hali hiyo inapojitokeza ndiyo inayotajwa kudhorotesha umakini wa mtu na kumfanya afanye kazi zake kama ‘msanii’ anayeigiza na hivyo kuathiri utendakazi wake.
Wakati nafanya uchunguzi wangu kwa kuoanisha na ule wa watafiti wengine wa kimatafa ukiwemo wa Dr. Irva Hertz-Picciotto, kutoka Chuo cha Carifonia Marekani, nilibaini pia viashiria vingine vya ufanisi duni wa kimasomo kutoka shule za jinsia moja na zile za mchanganyiko, ambapo uchunguzi unaonyesha kuwa wavulana wanaosoma shule huku wakiwa na uhusiano wa karibu na wasichana warembo huathirika kisaikolojia.
Hata hivyo, upo ushahidi mwingine kwamba kiwango cha kufaulu cha shule mchanganyiko kuwa chini kuliko wa shule za wasichana au wavulana peke yao, katika kulithibitisha hili mazingira ya shule na malezi yanazingatiwa.
Katika kumbukumbu iliyowashangaza wanasaikolojia na watafiti wa chuo cha Radboud cha Netherland ni pale mmoja wao aliposhindwa kukumbuka na kumwelekeza msichana mwenye mvuto aliyekutanishwa naye ramani ya eneo analoishi, jambo ambalo wenzake walisema lilitokea kwa sababu alikuwa kwenye mhemko wa hisia za kimapenzi.
Utafiti wao huo ulihusisha pia watu wengine na matokeo yalionyesha udhaifu mwingi kwa wanaume, huku wanawake wakiwa na kiwango kidogo cha kuathirika kwa kukutanishwa na wavulana wenye mvuto.
Ingawa si jambo la hatari sana kufikia hatua ya kulitangaza moja kwa moja kuwa ushirikishwaji wa wanaume na wanawake warembo katika ofisi, masomo na kazi mbali mbali una madhara lakini kitaalamu imebainika kuwa ni vema kundi linaloathirika ambalo ni sawa na asilimia 19 ya wanaume wote likapewa elimu ili kupunguza zaidi madhara ya kisaikolojia.
Changamoto hii, inamtaka kila mwanaume kupima mwenyewe mhemko wa nguvu za warembo kwa kujiuliza maswali ambayo yatamuwezesha kujua kama yuko kwenye kundi la wanaume wanaoweza kuathirika kisaikolojia kwa kufanya kazi na wanawake wenye mvuto au la! Lengo likiwa ni kuchukua hatua za kujikinga na madhara ya kisaikolojia.
Mwanasaikolojia Dr George Fieldman anakumbusha kitu muhimu alichokipa jina la ‘Reproductively Focused’ kuwa ndiyo sumu kali inayowadhuru wanaume wengi wanapokutana au kukutanishwa na wanawake wenye mvuto. Inaelezwa kuwa wanaume wanaovamiwa haraka na hisia za kimapenzi ndiyo wanaoweza kupata madhara ninayoyaeleza kwa kiwango kikubwa.
Itaendelea wiki ijayo.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter