KATIKA hali iliyowashtua watu wengi, kijana mmoja mkazi wa Ogun State Nchini NIGERIA amekamatwa usiku wa manane akiwa na katika shughuli nzito ya kufukua MAITI.
Katika mahojiano na Polisi mhalifu huyo ambaye alitambulika kwa jina la Jimoh alikiri kutenda kosa hilo, hivyo kufunguliwa mashtaka
Na katika kile kilichoonekana kama ni kichekesho ni pale bwana huyo alipohojiwa na POLISI na kusema
yafuatayo: " Kila mwanandamu anaruhusiwa kufanya kitu chochote ambacho kitaweza kumletea maslahi, Na hii ndio njia pekee ya mimi kuniingizia kipato na kukidhi mahitaji mengine kama mwanadamu " Alisema Jimoh
Hata hivyo Polisi nchini humo wameamua kulichukulia jambo hili kwa Busara zaidi ili kuepusha hisia chafu miongoni mwa jamii inayomzunguka Jimoh
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....