"DIAMOND NA WEMA SEPETU WAMERUDIANA...." NI MOVIE KWELI AMA PUBLICITY STUNT?


Diamond Wema-1
Let’s face this big elephant in the room…Diamond Platnumz na Wema Sepetu wana agenda ya siri. Naiita agenda ya siri kwakuwa kuna maswali makubwa mawili ambayo mimi na watu wengine wengi tunahisi Diamond anakificha kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu.
Swali la kwanza ni Diamond na Wema wamerudiana tena? Jibu la swali hili lilitolewa juzi na Diamond mwenyewe:
Kumekuwa na uvumi na habari nyingi sana mitandaoni na kwenye media tofauti… kwamba mimi na mwanadada Wema Sepetu tuna mahusiano ya kimapenzi, kitu ambacho sikweli na taarifa hizo ni za uongo.. uvumi huu ulianza kisa tu yeye kucomment kwenye account yangu ya instagram?..Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko kimahusiano ya mapenzi basi msizungumze ama kushiriki kwa chochote? Futeni huo uzamani na mbadilike, ina maana mnapenda kuona watu wanauadui… Ni muda wa kufanya kazi ili kulipa sifa na heshima taifa la Tanzania na si kuekeana chuki zisizo na faida..I real love my Penny,sijarudiana na Wema.”
Baada ya Diamond kuandika hivyo, swali hilo likaanza kupotea.
Lakini jana na leo swali hilo limekuja tena kwa kasi baada ya kuonekana picha mpya za Diamond na Wema Sepetu wakiwa pamoja katika nchi ya barani Asia ambayo bila shaka ni Malaysia ambako Diamond alikuwa ameenda kufanya show. Kwa picha hizo ni wazi, Diamond na Wema walienda pamoja. Picha za wapenzi hao wa zamani zimesambaa kwenye akaunti ya Instagram ya msichana anayejiita Chynabongo na sasa zimeshasambaa kama kila kona.

Diamond n wema
Baadaye Diamond naye akaweka picha moja kati ya hizo zilizowekwa na Chyna na kama kawaida yake akasema ni movie mpya inakuja.


“Katika moja ya muvie ambazo naimani itakuwa ni Gumzo, Mfano na Bora toka Tanzania basi ni hii… #TEMPTATIONS …. STAY TUNED!!!! SOON!….#DayOne #Location #SomeWhere,” ameandika.
Kufanya movie ni kisingizio nambari moja cha Diamond. Nikukumbushe kuwa kabla ya uhusiano wake na Penny kufahamika, ilileak picha yao wakionekana wakiwa wamelala, na wote kwa pamoja wakadai walikuwa location wakifanya movie mpya, ambayo hadi leo haijaingia sokoni... tutaingoja hadi miguu iingie tumboni.
Kufanyika kwa movie ya Diamond na Wema si kitu kigeni kusikika kwani tangu mwaka jana kulikuwa na taarifa hizo na tayari ilidaiwa walikuwa wameshalipwa. Kama watu wengine, nashindwa kuamini kwa haraka kuwa picha hizi zina ukweli wowote kuhusu kisingizio cha Diamond kuwa hiyo ni movie. Hata hivyo hivi karibuni, Wema alisema ameandaa surprise kubwa kwa mashabiki wake, labda hii ndio yenyewe basi…
“What more can I say other than thank ol my beloved fans for all da love nd support uve bin showing me nd naamini hamtoacha maana you guys are jus amazing…. kuna kitu nataka kufanya jus to show my appreciation… its a Surprise I wont tel… ila im sure y’all are gon die… nat die die, but y’all are gon b soooo happy… nawapenda mpaka basi…. thank y’all sooo much,” aliandika Wema kwenye Instagram.
Kama Wema na Diamond hawajarudiana, basi wawili hawa wanajua kucheza vizuri na akili za watu na uwezo huo ndio umewafanya wasiwe na mpinzani katika kutafuta ‘publicity stunts’. Uwezo huo ndio umewafanya wawe mastaa wanaongoza kwa kutawala kwenye magazeti ya udaku.
Picha hiyo ya Diamond na Wema imeshavutia comments zaidi ya 500 na like zaidi ya 2, 000 kwenye Instagram, na kwenye Facebook imepata comments zaidi ya 400 na likes zaidi ya 900 kwenye Facebook. I guess that what’s Diamond likes right? Confusing people’s minds.. and he is good at it. Na sasa tayari, Wema na Diamond wanatrend tena…kila website/blog leo ina habari yao.… mission accomplished.
Okay, tunaisubiria Temptations kwa hamu kubwa lakini tusije kuisubiria kwa muda mrefu kama tunavyoendelea kuisubiria ile ya Diamond na Penny.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter