LAANA: BUNGE NCHINI NEW ZEALAND LAIDHINISHA NDOA YA JINSIA MOJA....!!


Baadhi ya raia wanchi hiyo wakishangilia baada ya Bunge lao kuhalalisha ndoa ya jinsia moja.
 
Mamia ya watetezi wa haki za mashoga nchini New Zealand wamefurahia hatua ya uamuzi wa bunge la nchi hiyo wa kuhalalisha ndoa za jinsia sawa.
 
New Zealand imekuwa nchi ya 13 duniani na ya  kwanza katika eneo la Asia-Pasifik kuchukua hatua  hiyo.
 
Wabunge 77 walipiga kura kuunga mkono mswada huo na 44 waliupinga baada ya kuwasilishwa bungeni kwa mara ya tatu na ya mwisho.
 
Wananchi waliokuwa wamekaa katika sehemu ya wageni bungeni, pamoja na wabunge wenyewe walianza kuimba mara baada ya uamuzi  kutangazwa.
 
Hata hivyo watu wengi nchini New Zealand wanapinga ndoa za jinsia moja.
 
Kundi la wapiga debe-linaloitwa “Family First” mwaka jana liliwasilisha hati ya malalamiko bungeni, iliyotiwa saini na watu nusu milioni kupinga mswada juu ya kuhalalisha ndoa za mashoga

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter