WANAFUNZI wawili wa chuo cha biashara  wamepoteza  CBE 
wamekufa papo hapo kwenye ajali baada ya kugonga tela la mizigo 
lililokwama barabarani baada ya kuhalibika.
Ajali
 hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya kugonga tela la 
lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa wakitokea 
kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika kijiji cha 
ihumwa manispaa ya Dodoma.
Gazeti hili
 lilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo iliyopo 
pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa takribani saa zaidi ya tatu 
kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika na kuongoza utaratibu wa 
kuondoka.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa
 wa Dodoma Suzan Kaganda alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa
 wanafunzi hao wakati wakiendesha pikipiki hiyo  yenye namba za usajili T
 420 CCN  waliokuwa wakukitokea barabara ya morogoro kuingia mjini.
Suzan
 aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala wanafunzi wa CBE  
na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 477 ABM
 na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya wiki bala
 kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara hiyo yakiendelea katik
 eneo hilo.
Aliongeza kuwa miili ya 
marehemu hao iliyokuwa imehalibika vibaya kutokana na kufumuka fuvu la 
kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo  na ubongo kusambaa katika 
eneo hilo imehifadhiwa katika hospital ya mkoa.
Kwa picha za ajali hiyo bofya soma zaidi
lakini tunaomba radhi kwa picha hizo zinaleta usumbufu ukiziangalia

 Miili ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya kuondolewa katika kijiji cha Ihumwa barabara ya Morogoro Dodoma kabala ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.

 Baadhi
 ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma  walikufa kutokana
 na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi huku lori 
hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote barabarani 
hapo.

 Baadhi
 ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa msaada 
katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha biashara
 CBE Dodoma.

 Asikari
 wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa barabara sehemu 
ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la mizigo.



0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....