Imeelezwa
kuwa ufaulu wa mtihani wa kumaliza darasa la saba kwa mwaka 2013
umepanda kwa masomo yote kwa asilimia 19.89 ikilinganishwa na ilivyokuwa
kwa mwaka uliopita.
Kwamba,
wakati mwaka jana wahitimu waliopata asilimia 100 walikuwa asilimia
30.72, mwaka huu wameongezeka kuwa asilimia 50.61. Pia, somo ambalo
watahiniwa hao wamefaulu zaidi katika mtihani wao ni Kiswahili ambapo
ufaulu ni
asilimia 69.06 huku wakiwa wamefeli zaidi kwenye somo la Hisabati ambalo ufaulu upo chini kwa asilimia 28.62.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles
Msonde alisema wanafunzi 427,606 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya
msingi mwaka 2013 huku kiwango cha udanganyifu kikizidi kudhibitiwa
hivyo kupungua.
Alisema
NECTA imefuta matokeo yote ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa
watahiniwa 13, ambao walibainika kufanya udanganyifu kwenye mtihani au
kurudia pasipo ruhusa ya Baraza. Watahiniwa waliofutiwa mwaka jana ni
293.
Alisema
kati ya wanafunzi hao, 844,938 waliofanya mtihani huo wamepata alama
zaidi ya 100 katika alama 250: “Idadi hiyo ni sawa na asilimia 50.61.
Kati yao wasichana walikuwa 208,227 (sawa na asilimia 46.68) na wavulana
219,379 sawa na asilimia 55.01,” alisema.
Dk.
Msonde alisema katika ufanyaji wa mtihani huo, pia walikuwepo watu
wenye ulemavu, ambapo wasichana walikuwa 219 na wavulana 257.
Alisema
matokeo hayo yatapelekwa maeneo yote husika ili mchakato wa upangaji
shule ukifanyika kwa watahiniwa wote waliofaulu mtihani huo wa kumaliza
elimu ya msingi.
Kuhusu
usahihishaji mitihani, Dk. Msonde alisema ili kujiridhisha na usahihi
wa zoezi la usahihishaji wa kutumia mfumo wa kompyuta (Optical Mark
Reader - OMR), sampuli za karatasi 20,795 za majibu ya watahiniwa wa
shule 200 kutoka wilaya 48 zilichukuliwa kutoka shule za mikoa tisa ya
(Iringa, Kagera, Shinyanga, Manyara, Njombe, Mbeya, Morogoro, Katavi na
Tanga) na kusahihishwa kwa mkono: “Ulinganifu baina ya alama za
watahiniwa zilizopatikana kwa kusahihishwa kwa mkono na zile
zilizotokana na usahihishaji wa mfumo wa kompyuta ulifanyika na kubaini
kompyuta ilikuwa sahihi,”alisema.
Amesema
makosa yaliyojitokeza katika karatasi zilizosahihishwa kwa mkono ni
kuweka pata pale ambapo kuna kosa ama kuweka kosa pale ambapo kuna pata,
makosa ambayo kwenye usahihishaji wa kutumia kompyuta hakuwepo.
Matokeo ya dalasa la saba yaliyopachikwa hapo juu pia yanapatikana katika tovuti za:
HAYA NDO MATOKEO YENYEWE
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....