
MBUNGE wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), ameingia katika matata. Katika kujaribu kudhibiti mtoto wa shule ambaye anadai alibakwa naye na kuambukiwa virusi vya ukimwi, mbunge huyo ametoa vitisho vya kuua mtoto huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili.
  Siku moja baada ya gazeti  la  Tanzania Daima  kuripoti habari za mbunge mmoja (bila 
kumtaja jina), jana asubuhi Profesa  Kapuya ameibuka na kumtisha 
mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 anayesoma Shule ya  Sekondari Turiani 
iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam.
  Baada ya kujua kuwa mtoto  huyo ndiye alitoa habari za masahibu hayo, 
ambayo mbunge hakutaka yajulikane,  alimpigia simu mtoto huyo, na 
baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.
  Jana Tanzania Daima  ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Profesa Kapuya kwenda kwa  mtoto huyo.
  Alfajiri saa 11:21 kupitia  simu yake ya mkononi yenye namba 
0784993***, Profesa Kapuya alituma ujumbe  ufuatao kwa mtoto huyo: 
“chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?”
  Baadaye saa 1:07 asubuhi,  alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo 
hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: “Mkiuawa,  itakuwa nzuri, 
itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali,  mtoto 
mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.
  “Mwambieni Mbowe mwenye  hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si 
mmemuingizia hela leo? Mnatumika bure  watu wanaingiza hela nyingi, 
mmenitibua lazima niwauwe wiki hiii haitaisha,  nitapanga kambi popote.
  “Jana si wamekuficha? Tuone  kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa 
imeisha, maana wameshatengeneza hela. Lazima  mvae sanda. Hilo sio ombi,
 ni wajibu wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto  wetu wanauza unga, 
nani anawakamata? Nani atapigana nasi?”
  Hata hivyo, baada ya  kuhisi kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia 
hatua, na wamewasiliana na  taasisi mbalimbali za kiraia na serikali 
zenye uwezo wa kumtia adabu, mbunge  huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa
 kuonyesha alikuwa anafikiria kunywa sumu..
  Ujumbe huo uliotumwa kwa  mtoto huyo saa 11:2 3 ulisema: “nimewakosea 
sana, acha nife mie nakunywa sumu  nijiue, na nyie mje mnizike.”
  Hasira za Profesa Kapuya  dhidi ya mtoto hao zilitokana na hatua ya 
mtoto huyo na dada yake kufichua  unyama wanaodai kutendewa na mbunge 
huyo, ambaye amewahi kushika nyadhifa  kadhaa za uwaziri katika Serikali
 ya Awamu ya Nne.
  Tangu alipogundua kuwa  mtoto huyo alizungumza na gazeti hili juzi, 
saa 5:17 usiku wa kuamkia jana  alituma ujumbe usemao: “Si mpo Bilz? 
Sasa tupo pamoja na nyie mpaka usiku.”
Baadaye saa 5:31 alituma  ujumbe  huu: “Hivi hamkubali kushindwa?  Leo ulifuata nini ofisi ya CCM?”
  Ujumbe huo ulitokana na  ukweli kwamba dada wa mtoto anayedaiwa 
kubakwa alifika Makao Makuu ya Chama Cha  Mapinduzi (CCM) juzi asubuhi 
kuonana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman  Kinana, ili kuomba 
chama kimsaidie kumbana Profesa Kapuya, ambaye alikuwa  ameanza 
kuwatisha yeye na mdogo wake.
  Hata hivyo, kwa mujibu wa  mtoto huyo, Kinana alisema suala hilo si la chama bali la Profesa Kapuya  binafsi.
  Mtoto huyo alikataa  ushauri wa kupeleka shauri hilo mbele ya vyombo 
vya sheria, akidai kuwa jitihada  zake zimekuwa zinazimwa na mbunge huyo
 anayedai serikali haiwezi kumfanya  lolote.
  Alisisitiza kuwa hana  imani na serikali, lakini akasema yupo tayari 
kuchukua hatua kali dhidi ya  Profesa Kapuya iwapo atasimamiwa na 
watetezi wa haki za binadamu.
  Baadhi ya mashirika  yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha 
Sheria na Haki za BInadamu (LHRC)  na Mtandao wa Kijinsia Tanzania 
(TGNP) yalijitokeza kumsaidia watoto hao, ambao  ni yatima.
  Mtoto huyo na dada yake, wakizungumza  na gazeti hili kwa hofu 
mafichoni, walisema kwa sasa hawana imani tena kama  kuna serikali 
nchini Tanzania kwa kuwa wamedhalilishwa, wametembezwa hadi  Bungeni na 
wabunge bila hatua kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika kituo  cha
 polisi Oysterbay tangu mwaka jana.
  Hata hivyo, kabla ya tukio  la watoto hao kuripoti, ofisi za gazeti 
hili juzi usiku kulikuwa na watu  waliokuja wakiwatafuta watoto hao, 
huku wakiwatisha kwa simu na kuwatolea  maneno ya kejeli, wakidai 
watawamwagia tindikali.
  Mmoja wa watoto hao,  alidai kuwa miongoni mwa vijana waliokuwa 
wanawatisha juzi walikuwa katika gari  T170 BGY, Benz, Cream Metalic, 
ambayo inamilikiwa na mbaya wao.
Jana gazeti  hili  lilichapisha habari kuwa  mwanafunzi huyo 
aliyesema kuwa waziri  huyo  alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii 
iliyoko jijini Dar es Salaam  mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho 
katika Jengo la Biashara Complex  lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 
alipoitwa kwenda kuchua ada kwa mara ya pili. 
  Akizungumza kwa uchungu,  alisema mbunge huyo alifanya kitendo hicho 
kwenye Hoteli ya Giraffe, Jijini Dar  es Salaam mwaka 2011.
  Alisema kuwa yeye alikuwa  na urafiki na mwanafunzi mwenzake Zuhura 
Mwaking’inda. Mwaking’inda amewahi  kuwa Diwani wa Kata ya Sinza Jimbo 
la Ubungo, Jijini Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa mwanafunzi  huyo, rafiki yake (mtoto wa Mwaking’ida) 
alikuwa amepooza hivyo alikuwa  analazimika kumhudumia hali 
iliyowaunganisha hadi huyo mtoto alipochukua jukumu  la kumtambulisha 
kwa baba yake ambaye naye alimtambulisha kwa Kapuya ili aweze  kumsaidia
 fedha kwa jili ada.
  Mwanafunzi huyo alisema  baada ya kutambulishwa aliitwa katika hoteli 
moja jijini Dar ambapo baada ya  kufika mapokezi wafanyakazi wa  hoteli 
hiyo walimkataza kuingia chumbani  katika maana kwamba umri wake alikuwa
 mdogo (mwaka 2011 alikuwa na miaka 14),  lakini Kapuya aliamrisha aje 
chumbani pamoja na dereva na kumwingiza kwa nguvu.
  Akiwa chumbani alimlazimisha kulala naye kisha  kumpa sh laki saba, 
badala ya sh elfu sitini na saba kiasi ambacho kilikuwa  ndio mahitaji 
halisi ya ada.
  Mwanafunzi huyo amesema  baada ya muhula mmoja aliitwa tena na mbunge 
huyo katika Jengo la Biashara  Complex lililoko Mwananyamala tarehe 3 
June 2012, ambapo pia alimlazimisha  kulala naye kwenye zulia la ofisi 
yake, kisha kumpa sh 350,000/.
  Alisimulia kwamba wakati  anatoka kwa huzuni ofisini kwa mbunge huyo, 
mmoja wa wahudumu wa hapo  alimuuliza kwanini anatoka kwa huzuni, 
alimweleza kisa hicho, na huyo mama  aliangua kilio kwa kumwambia 
“mwanangu umekufa pole tu, huyu baba ni muathirika  wa ukimwi”.
Aliongeza kuwa baada ya  kuambiwa vile alilia na kufanya fujo hapo 
mapokezi hadi alipokamatwa na walinzi  wa kisha kupelekwa kituo cha 
polisi kufunguliwa mashtaka, lakini akiwa polisi  alipoeleza mkasa wote,
 Polisi walilazimika kumwita Kapuya na wakawasuluhisha  kwa makubaliano 
kwamba Kapuya atakuwa anamlipia ada, na kumpa pesa za matumizi  sh. laki
 tatu kila mwezi, jambo ambalo amekuwa akilitekeleza kupitia simu yake  
ya mkononi 0755993***.
  
 Kwa mujibu wa mwanafunzi  huyo, 24 Januari 2013, alifika mtu 
nyumbani kwao mtu mmoja (jina tunalihifadhi)  na kujitambulisha kuwa 
yeye ni jambazi na kuwa alitumwa kwenda kuwaua kwa  malipo ya sh. 
milioni 50, lakini alipokuta ni watoto wadogo aliwasamehe, na  kusema 
yeye ni jambazi sugu hawezi kupoteza nguvu zake kuua vitoto.
  Alienda akiwa na bastola,  maji kwenye chupa yanayodhaniwa kuwa ni 
tindikali na bomba la sindano. Kwa  mujibu wa mtoto huyo, jambazi huyo 
anasema kuwa tayari alilipwa milioni 15 za  awali.
  Mtoto huyo alisema jambazi  huyo aliwambia kuwa yeye ni rafiki wa 
mtoto wa Kapuya na wanamfahamu vizuri,  lakini hataweza kuaua baada ya 
kubaini kuwa wao ni yatima tu.
  Hata hivyo kufikia mwezi Februari  mwaka huu, mtu asiyefahamika 
alienda nyumbani na kutelekeza gari aina ya T.199  BGY Mercedes Benzi ya
 Blue wakati wanafunzi hao wakiwa shuleni, kisha kuacha  ufunguo kwa 
jirani yao kwa maelekezo kuwa wakifika awapatie.
  
  Na Kapuya aliwapigia simu  kuwaarifu kuwa amempa zawadi ya gari kwa 
ajili ya matumizi ila yeye na dada  yake wanaruhusiwa kuuza ili wapate 
pesa kwa ajili ya mahitaji yake siku  zilizosalia, kwani muda sio mrefu 
baada ya uchguzi mkuu 2015, Kapuya atakuwa  Waziri Mkuu, hivyo itakuwa 
ngumu yeye kumtumia huyo binti pesa kama  alivyoelekezwa na jeshi la 
polisi kituo cha Oysterbay.
  Baada ya mwanafunzi huyo  na dada yake ambaye ana umri wa miaka 20, 
kupewa gari walishindwa kulitumia hivyo  kutoa taarifa polisi kwani kwa 
kupokea gari hilo  ilikuwa ni kuwatelekeza kwani yeye hana hata  hela ya
 kuweka mafuta ya gari, hivyo walienda polisi ili kesi ipelekwe  
mahakamani kumshtaki kapuya.
Polisi wa Oysterbay  walikubali kulipeleka tatizo hilo kwa Katibu wa 
Bunge, ambaye alimwita  mwanafunzi huyo na mdogo wake waende Dodoma 
kukutana na Kamati ya Haki, Maadili  na Madaraka ya Bunge ingawa 
walipofika Dodoma walikaa na kamati ya hiyo kwa  maelezo kuwa Kapuya 
hakuwepo hadi Bunge lilipoisha walirejeshwa Dar es Salaam.
  Mtoto huyo na dada yake  alitoka ofisi za CCM lakini akiwa anaelekea 
kituo cha basi alithadharishwa na mwanafunzi  mwingine kwa haraka kuwa 
akimbie kwa kuwa atamwagiwa tindikali na watu  waliokuwa wanamfuata 
nyuma, alikimbilia katika mtaa wa Hoteli ya Star  light kisha aliomba 
msaada baada ya kupotea njia na hivyo alisaidiwa na mama  mmoja 
kufikishwa chumba cha habari cha Channel Ten.
  Ni katika chumba hicho  ndio mwandishi wa habari hizi alienda na 
kuwakuta watu wawili hao waliokuwa  wanamhitaji binti huyo lakini 
walikatazwa kumchukua.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima



Hii inaonesha serikali yetu ilivyokuwa haifuatilii madhambi ya viongozi wake,.....ni uuaji kushindwa kumkamata mtu (Kapuya) anayeeneza virusi vya ukimwi makusudi, naomba mashirika ya hiari ya kutetea na kulinda haki za binadamu hasa watoto kama hao yafuatilie mkasa huu na kumutia adabu filauni kapuya.
ReplyDeleteHizi habari kama za kutungwa mana mtoto alibakwa 2011 mpaka sasa 2yrs alikua wapi? Na pesa zilimnogea baada ya kuambiwa mzee kapuya ana ngoma ndo kaamua atangaze mbona amechelewa. Watoto achenini kupapalika na mboo za kizee kwa tamaa ya cku moja na gonjwa la milele
ReplyDeletehuyu binti nae ana makosa mtu atakubakaje mara mbili? na anaonekana ni kurumbembe mtoto under 18 alifuata nini club bilz?
ReplyDelete