MASTAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka na Wema Sepetu wanadaiwa kuingia 
vitani, mpambe mmoja wa Wema akitumia mtandao wa kijamii wa Instagram 
alimtuhumu Rose kwamba aliwahi kushiriki kikao kimoja kilichokuwa 
kikimjadili ‘madam’ huyo sanjari na kumtukana.
Mpambe huyo aliyetumia picha ya Wema (huenda akawa Wema mwenyewe), 
alisema kuwa siku moja isiyokuwa na jina hivi karibuni, Rose alishiriki 
kikao hicho kilichofanyika kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es 
Salaam ambapo sehemu kubwa ya mazungumzo ilikuwa ikimchambua Wema.
Akizungumza na Amani kwa njia ya simu juzi kuhusiana na tuhuma hizo, 
Rose alisema anashangaa matusi anayotukanwa na mtu huyo kwani ana mwaka 
mmoja hajawahi kukanyaga katikia viwanja hivyo vilivyopo Kinondoni, Dar.
“Kiukweli huyo mtu amenitukana bure, hajakaa na kufanyia uchunguzi 
hizo taarifa alizopewa, mimi sikumbuki kama kuna siku niliwahi kukaa 
Leaders na kuanza kumsema vibaya Wema kwani nina mwaka sijawahi kufika 
Leaders.
“Binafsi sina muda huo wa kumzungumzia mtu au kukaa na mtu ambaye 
hana faida kwangu. Mimi rafiki yangu ni mchumba wangu (Malick Bandawe), 
mama yangu na ndugu zangu zaidi ya hapo tunakutana shutingi tukimaliza 
narudi kwangu, namsihi huyo mpambe wa Wema afanye tena uchunguzi,” 
alisema Rose.
Juzi, Amani lilimsaka Wema kwa njia ya simu ya mkononi ili azungumzie
 madai hao lakini hakupatikana. Hata hivyo, habari zinasema kuwa mtu 
aliyemtukana Rose kwenye mtandao alitumwa na Wema au Wema mwenyewe.
Tangu Diamond kurudiana na Wema na kusambaza picha zao katika 
mitandao ya kijamii, hivi karibuni Wema kufiwa na baba yake mzazi (Isaac
 Sepetu) na baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi kususia msiba huo, kumeibuka
 makundi ya watu kazi yao kubwa ni kutukana watu ambao wako tofauti na 
Wema----CREDIT: GPL



0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....