Watuhumiwa
wawili wa kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Wilaya ya Rungwe, John Mwankenja, Kelvin Myovela(kushoto),
aliyehukumiwa kifungo cha miaka saba jela na David Mwasipasa(Kulia)
amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia katika
Mahakama kuu kanda ya Mbeya.
Mhukumiwa
namba moja wa kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Hakimu Mwakalinga(kushoto) amehukumiwa
kunyongwa hadi kufa na mwenyeshati la Bluu ni Obote Mwanyingili
amehukumiwa miaka saba jela kwa kumhifadhi mtuhumiwa.(Picha na Ezekiel
Kamanga, Mbeya)
Awali
kabla ya kusoma kwa hukumu hiyo Mwendesha mashtaka wa Serikali.,
Archiles Mulisa, aliwataja watuhumiwa wote wanne kuwa ni Hakimu
Mwakalinga, Daudi Mwasipasa, Obote Mwanyingili na Kelvin Myovela
wanaokabiliwa na tuhuma za kumuua kwa maksudi aliyekuwa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe John Mwankenja.
Alisema
watuhumiwa hao wenye kesi namba 131/2012 walitenda kosa hilo Mei 19,
2011 katika kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe
Mkoani Mbeya.
Mulisa
aliyekuwa akisaidiwa na Wakili wa Serikali Lugano Mwakilasa kwa upande
wa mashtaka huku Watuhumiwa wakitetewa na Mawakili wawili ambao ni
Victor Mkumbe na Simon Mwakolo.
Mulisa
alidai mahakamani hapo kuwa kesi inayowakabili watuhumiwa hao
walilitenda Mei 19,2011 kwa kumuua kwa maksudi John Mwankenja kinyume na
kifungu cha 196 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Akisoma
hukumu hiyo Jaji Karua ambaye alianza majira ya saa 14:37 mchana na
kukamilisha saa 15:37 alisema katika kesi hiyo upande wa mashtaka na
utetezi haubishaniwi kuhusu kifo cha marehemu.
Aliongeza
kuwa pande hizo mbili pia hazibishaniwi kuhusu ripoti za kitaalamu na
dhamira za mauaji hayo bali kinachobishaniwa ni uhusika wa watuhumiwa
hao dhidi ya mauaji hayo.
Alisema
katika kutetea hoja zao upande wa mashtaka ulileta mashahidi 11 ambao
wote kwa pamoja wakiongozwa na shahidi namba moja waliwatuhumu
washtakiwa kuhusika na tukio hilo.
Shahidi
huyo namba moja Weston Jacob(17) mkazi wa Kiwira Mwanafunzi kidato cha
Tatu katika shule ya Sekondari Kipoke ambaye pia ni Mjomba wa marehemu
ambaye aliiambia mahakama kuwa siku ya tukio akiwa nyumbani akijisomea
majira ya 2: 30 usiku ambapo marehemu alifika nyumbani na kupiga honi ya
gari akitaka afunguliwe mlango.
Mbali
na ushahidi huo Jaji Karua alisema pamoja na ushauri wa wazee wa baraza
la mahakama ambao pia wanawatuhumu washtakiwa hao kuhusika na tukio
hilo nae anakubaliana nao lakini siyo kwa watuhumiwa wote.
Kutokana
na ushahidi huo alisema Mshtakiwa namba moja na namba mbili ambao ni
Hakimu Mwakalinga na Daudi Mwasipasa wanatiwa hatiani kuhusika moja kwa
moja na mauaji kutokana na ukiri wao kwa mlinzi wa amani, Mchukua
maelezo na vipimo vya vinasaba.
Alisema
Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili yeye anatiwa hatiani kutokana na
kosa la kumhifadhi mtuhumiwa namba moja baada ya kutoka kufanya mauaji
hivyo yeye hausiki moja kwa moja na kosa hilo.
Jaji
karua alisema kwa upande wa mshtakiwa namba nne Kelvin Myovela anatiwa
hatiani kutokana na kuhifadhi silaha iliyotumika nkatika mauaji hayo
ingawa hakusika na kitendo hicho moja kwa moja.
Aliongeza
kuwa kutokana na kifungu cha sheria cha mwenendo wa makosa ya jinai
kifungu namba 300 na 217 washtakiwa namba tatu na namba nne wanatiwa
hatiani na mahakama.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa, aliiambia mahakama hiyo kwamba
itoe adhabu kali kutokana na kitendo alichofanyiwa marehemu na iwe
fundisho kwa watu wengine.
Kwa
upande wa utetezi ambao siku ya hukumu uliwakilishwa na Wakili Merick
Luvinga alisema mahakama iwanee huruma washtakiwa kwa kuwa wote umri wao
ni mdogo wanaweza kujifunza na kurudi kuungana na jamii pia ni kosa lao
la kwanza hivyo wasipewe adhabu kali.
Kutokana
na utetezi huo, Jaji Karua alisema kutokana na ushahidi uliotolewa
mahakamani hapo kuthibitisha kuhusika pasipo shaka kwa washtakiwa namba
moja na namba mbili hivyo adhabu yao ni kunyongwa hadi kufa.
Aliongeza
kuwa Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili anayehusika kumhifadhi
mtuhumiwa wa kwanza ataenda jela miaka saba kwa kosa hilo sambamba na
mshtakiwa namba nne Kelvin Myovela aliyehifadhi silaha iliyotumika
kwenye mauaji.
Alisema
kutokana kosa hilo mtuhumiwa huyo atatumikia kifungo jela miaka saba
ingawa pia tayari alikuwa amehukumiwa kifungo jela cha miaka 20 kwa kosa
la kukutwa na silaha kinyume cha sheria.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....