VIDEO:AFARIKI KWA KUKOSA HEWA BAADA YA TANKI LA MAFUTA KULIPUKA....


ITV imeshuhudia jitihada za jeshi la polisi na kikosi cha zimamoto na uokoaji wakishirikiana na wananchi katika kuondoa mwili wa marehemu ambapo wakizungumzia tukio hilo baadhi ya mashuhuda wamesema  marehemu alikuwa akichomelea vyuma ndani ya tenki hilo lililokuwa limeharibika ambapo ghafla ulitokea mlipuko na kupelekea marehemu kukosa hewa ingawa  jitihada za kumtoa akiwa Hai zilishindikana kutokana na kukosa hewa.

Kwa upande wake mwakilishi wa zamu wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Morogoro Masoud Ramadhan amesema uchunguzi wa haraka uliofanyika umebaini  kuwa baada ya kutokea mlipuko uliosababishwa  harufu kali ya mafuta ndani ya tank hilo na ambapo mamehemu alikosa hewa

Mwili wa marehemu umechukuliwa na jeshi la polisi na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro 


Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter