WATU wawili wameripotiwa kufariki dunia jijini Dar es Salaam katika matukio mawili tofauti akiwamo mzazi aliyejirusha kutoka ghorofani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieth Mnangi, alisema jana kuwa mzazi huyo, Lewana Melkiory (38) mkazi wa Sinza, alijirusha kutoka wodi ya wazazi ghorofa ya pili juzi usiku na kufariki dunia papo hapo.
Alisema mwanamke huyo alijifungua Oktoba Mosi na kulazwa hospitalini hapo na mtoto wake.Kamanda Marieth alisema sababu za kujirusha kwa mwanamke huyo hazijafahamika, na maiti imehifadhiwa hospitalini hapo.
Katika tukio jingine, dereva wa pikipiki T 774 CKK Fekon aliyefahamika kwa jina la utani Kwea pipa, amefariki dunia baada ya kugongana uso kwa uso na gari lisilofahamika.
Ajali hiyo ilitokea juzi, barabara ya Kitunda, eneo la Hali ya Hewa TANESCO.
Abiria katika pikipiki hiyo, Robiso Hamazima (21) mkazi wa Ubungo, alijeruhiwa na amelazwa hospitali ya Amana. Maiti imehifadhiwa hospitali ya Amana.
-Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....