Wananchi 6,700 wa Kata ya Kilolambwani wilayani hapa wanakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa chakula na kusababisha baadhi ya wananchi kula mizizi ya porini.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata hiyo, Salamu Matajabu pamoja na wenyeviti wa Serikali za Vijiji vya Nangole na Dimba wakati walipokuwa wanazungumza na timu ya waandishi wa habari kwa nyakati tofauti mjini Lindi jana.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Dimba, Abdalla Mbwana amesema hali ya chakula kwa wananchi wake ni mbaya jambo linaloweza kusababisha baadhi ya wakazi wa kijiji hicho kupoteza maisha kutokana na kukosa chakula.
Naye Diwani wa kata ya Kilolambwani Salamu Mtajabu alisema tatizo la njaa katika eneo hilo limevikumba vijiji saba vinavyounda kata hiyo lililosababishwa na ukosefu wa mvua kwa misimu miwili mfululizo wa 2010/11 na 2012/13.
Matajabu alisema zinahitajika juhudi za makusudi na haraka kuwapatia msaada wa chakula wananchi hao ili kuokoa maisha ya wakazi hao .
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk Nasoro Himidi alisema tatizo la upungufu wa chakula katika kata hiyo, ofisi yake inalitambua na tayari ameomba tani 19,000 za nafaka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Maafa .
Hata hivyo katika utafiti wa hivi karibuni imebainika kuwa takribani wa watu Milioni 840 wanakabiliwa na upungufu wa chakula duniani,huku watu bilioni 2 wakikabiliwa na tatizo la lishe na chakula bora wakati bilioni 7 wakiwa katika hatari ya kushambuliwa na utapia mlo duniani Afrika ikiongoza.
Sorce: Mwananchi
Sorce: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....