HOJA: KAMA WABUNGE WANAONGEA MATUSI BUNGENI, KWANINI WANAFUNZI WASICHORE MAZOMBI KWENYE MITIHANI YAO....?!!



Bunge letu linaelekea wapi jamani, Yaani wabunge waliopewa idhini na wananchi wao ili kutetea maslahi ya wananchi wao hivi sasa ndo wamekuwa viongozi wa kutukana matusi bungeni.

Vitendo hivi vya kusikitisha vinaonyesha dhahiri kuwa kwa sasa Elimu ya Uzalendo hapa Nchini kwetu inaelekea kupotea, Wimbo wa chuki na Udini umeonekana kutawala midomoni mwa Wengi hivi sasa.
Bunge ni moja kati ya sehemu tajwa hapa Nchini kwetu kuwa ni TUKUFU hivyo kila mmoja awapo mahala hapo inabidi kuheshimu na kutii Sheria na Mamlaka kama vile inavyowataka kufanya..

Hii ni hatari sana na binafsi nilianza kuingiwa na wasi wasi pale vuguvugu hili la kiupinzani ambao hauna manufaa kwetu sisi wananchi kuona waheshimiwa wabunge wanaligeuza Bunge kuwa kama sehemu ya kuvutia Bangi(kijiweni),

Kama ukiangalia kwa haraka haraka hata hoja ambazo zimekuwa zikijadiliwa ndani ya Bunge siku za hivi karibuni hazina tija kwa taifa letu pendwa la Tanzania.
Kama Waziri au Mbunge anaweza kupata Ujasiri na kusimama na kutoa hoja na changamoto kwa Serikali kuwekeza kwenye zao haramu la Bangi na huku swala hilo likibarikiwa na Naibu waziri wa Kilimo na chakula Adamu Malima kusema ITALIFANYIA KAZI WAZO LILITOLEWA BUNGENI NA MBUNGE WA CCM KUTAKA BANGI IHALALISHWE KULIMWA KIBIASHARA!! 

Hii ni hatari kabisa kwa kizazi chetu hiki....!!  Siku hizi imekuwa ni kitu cha kawaida kabisa kwa Mbunge kumtukana mbunge mwenzie, kwa mfano ukijaribu kuiangalia ile kauli ya Mheshimiwa Juma Nkamia akimwambia Mheshimiwa Joseph Mbilinyi  kuwa "SIONGEI NA MBWA, NAONGEA NA MWENYE MBWA"  .......Mnatupeleka wapi wawakilishi wetu jamani? hivi tuliwatuma mkatutetee Bungeni au kutudhihirishia tabia zenu ambazo mlizificha wakati mlipokuwa mnatuomba ridhaa yetu kipindi cha Uchaguzi??......Ama kama hiyo haitoshi mnaamua na kutukana matusi ambayo hatuwezi hata kufikiria kama yapo kwenye vinywa vyenu.Yaani mtu anakosa kabisa Namna ya kuwarekebisha wenzake Bungeni ambapo ni sehemu tukufu mpaka anaamua kutumia neno F*CK YOU, huku ni kulidhalilisha Bunge kupitiliza!! Mbunge ambaye aliongea hivi nadhani ingekuwa ni kipindi kile cha hayati Mwalimu Nyerere basi Tungemshuhudia akichapwa viboko Hadharani na kufukuzwa kabisa Bungeni.

Sasa swali Linakuja hivi kama Wabunge ambao Mnabeba Ridha za Wananchi wenu mnaamua kuongea matusi Bungeni,  kwanini  wanafunzi wachichore MAZOMBI na kuandika mashairi ya taarabu kwenye Mitihani yao...?!!!

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter