Una kipaji kinachokubalika kaka ila napenda kujua wewe ni mwenyeji wa wapi na una elimu gani? Kelletho, Dar, 0752250475
MAVOCO: Ni mwenyeji wa Morogoro, nina elimu ya kidato cha nne.
Rich Mavoco.
Rich mimi nakubali sana kazi zako lakini inadaiwa wewe Freemason, ni kweli? Issa Chongono, Tanga, 0714455748MAVOCO: Hapana siyo kweli.
Aoe mapema
Nakukubali ila nakushauri usitafute usupastaa kwa ajili ya wanawake kama hujaoa tafuta mke uoe. Amoni, Tanga, 0654016122
MAVOCO: Nashukuru ushauri wako nimeupokea.
Ushauri
Ebwana uko vizuri ila tatizo lenu ni moja kwa wote, majigambo mengi ila uwezo ni mdogo, wacheza shoo wengi na faida yake siioni ila komaa unajitahidi. Kuzza Nzagamba, 0715438585
MAVOCO: Nashukuru.
Asivimbe kichwa
Naipenda sana staili yako ya kuimba na hasa shoo zako, sidhani kama kuna msanii Tanzania anayekufikia, ushauri ongeza juhudi usivimbe kichwa. Julius Myinga, Iringa, 0754887651
MAVOCO: Nashukuru.
Malengo ya baadaYe
Nakukubali sana, nini malengo yako ya baadaye na umejipanga vipi kwa mashabiki wako maana muziki unakuwa kwa kasi? Kalemele, Dar, 0764147893
MAVOCO: Nina malengo ya kufanya muziki wa kimataifa zaidi na kupata watu wa kunisaidia kimuziki wenye uwezo mkubwa.
Huyu anaomba ndoa
Rich kama hujaoa mimi ningependa unioe, kabila langu ni Msukuma na mwenyewe ninajijua naamini nitakuvutia. Sabrina Ally, Moshi, 0754585773
MAVOCO: Asante sana ila umeshawahiwa, nina mchumba.
Kwa nini muziki?
Mavoco nini hasa kilikushawishi uwe mwanamuziki katika maisha yako? Msomaji, 0717651169
MAVOCO: Sababu kubwa nilijiona nina kipaji cha muziki, pia namshukuru Nuruel alinionyesha njia.
Ung’eng’e wake
Rich Mavoko Kiingereza chako ulichotumia kwenye wimbo wa Marry Me ni sahihi? Ernest Kidenya, Mbeya, 0713333776
MAVOCO: Ndiyo.
Kuhusu kologwa na Diamond
Mavoko upo juu, hivi ni kweli kutofanya vizuri katika shoo yako ya Fiesta ulilogwa na Diamond au? Dimo Love, Dar, 0653687666
MAVOCO: Hapana na mimi kama Rich Mavoko siamini.
Akaze buti
Waliotangulia wamelewa sifa, wewe unaweza kaza buti. Naomy, Dar, 0754435580
MAVOCO: Nitajitahidi kufikia lengo ili nisilewe sifa.
Nje ya muziki
Nakukubali sana Rich, je nje ya muziki unajishughulisha na nini? Zulpha, Karatu, 0653095356
MAVOCO: Nafanya biashara ndogondogo.
Eti alikuwa mpiga debe?
Mavoko ni kweli ulikuwa unapiga debe pale Madoto Mburahati? Msomaji, 0656540304
MAVOCO: Sijawahi.
Undugu na Tine White
Nakubali kazi zako, nilisikia una undugu na Tine White kuna ukweli wowote? Zai Mpute, Dar, 0656268473
MAVOCO: Ndiyo ni kaka yangu.
Kwa nini mapenzi zaidi?
Hongera sana kaka, unafanya kazi nzuri sana kwenye muziki, je kwa nini wasanii wengi mnapenda kutoa nyimbo za mapenzi zaidi? Winnie, Songea, 0714101527
MAVOCO: Mapenzi yameteka nusu ya dunia ndiyo maana.
Ni mtoto wa Kimamba?
Mavoco kweli wewe ni mtoto wa Kimamba Kilosa? Msomaji, 0716332868
MAVOCO: Ndiyo.
Kuhusu Diamond
Uko juu jembe, vipi kuhusu kushuka kiwango kwa Diamond nasikia wewe ndiye uliyechangia? Sharo, Zenji, 0776822230
MAVOCO: Siyo kweli na sijui kama Diamond anashuka, mimi napenda aendelee kuwepo.
Huyu anamjua kidogo
Ulishawahi kusoma Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja na unatoka na msichana mmoja anaitwa Aysher anakaa Magomeni Mwembechai. Msomaji, 0656397341
MAVOCO: Kweli nimesoma Mnazi Mmoja ila sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke anayeitwa Aysher.
Asiwe kama Diamond
Rich nakukubali sana mwana ila wosia wangu kwako, ukitaka uendelee mademu weka kando, usiwe kama Diamond. Selemani Alifa, Dar, 0718803204
MAVOCO: Nashukuru.
Kuhusu madawa ya kulevya
Wewe kama msanii mchanga unalichukuliaje suala la wasanii kuathirika na madawa ya kulevya? Neema, Dar, 0787183920
MAVOCO: Ni kitu kibaya kiukweli na chanzo kikiwa ni ushawishi kutoka kwa vijana wanaotoka sehemu moja ila wasanii tunalipiga vita sana.
Anatafuta umaarufu kupitia Diamond
Rich unatafuta umaarufu kupitia Diamond? Msomaji, 0719974662
MAVOKO: Haiwezekani kwa sababu kila mtu anafanya muziki.
Usumbufu wa mademu
Rich wewe ni msanii mahiri kunako anga la muziki wa kizazi kipya Bongo, je vipi kuhusu usumbufu wa mademu mcharuko? Salim Liundi, Dar, 0658110395
MAVOKO: Huwa sioni kama ni usumbufu kwa sababu mademu ni sehemu ya mashabiki wangu na ikitokea amenifuata msichana na kunitaka kimapenzi huwa natafuta jinsi ya kumkwepa.
Anawabania ‘andagarundi’
Mavoko wewe mkali hilo halina ubishi ila inasemekana huwa unawabania wasanii wachanga wakitaka kufanya kolabo na wewe, kwa nini? Riziki Minde, Dar, 0716000045
MAVOKO: Siyo kweli, mimi ndiye msanii niliyefanya kolabo nyingi sana na wasanii wachanga.
Kwa nini bifu?
Mavoko wewe ni mkali kaka ila kuna kitu sijakielewa, kwa nini wasanii mnaendekeza bifu ambazo hazina msingi? Edsony, Dar, 0717725430
MAVOKO: Sijawahi kuwa na bifu na mtu.
Asilewe sifa
Nakupongeza sana kwa kazi zako nzuri ila usilewe sifa ukapotea kama wakali wengine. Elia Msuya, Arusha, 0758509407
MAVOKO: Asante sana.
Kuhusu wizi wa wimbo wa Follow Me
Nakukubali sana Rich, vipi ukweli kuhusu wimbo wa Follow Me ni kweli ulimuimbia Dogo Chismo? Jagar, Dar, 0778384438
MAVOKO: Mashabiki zangu ndiyo muamue wenyewe nani mwizi, huyo dogo alikuwa densa wangu na alikuwa anapenda sana kuimba ndiyo akazusha kuwa nimemuibia wimbo huo.
Amuweke wazi shemeji yetu
Mavoko nakupenda sana, naomba siku moja utuambie shemeji ni nani maana ukiwa msanii mambo kibao kuhusu mademu usiwe kama Diamond. Imma, Mbeya, 0768567486
MAVOKO: Siku moja mtajua muda ukifika wala msijali mashabiki zangu.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....