Majina ya Diamond na Lady Jaydee yanaweza kuwa miongoni mwa majina ya wasanii wa Tanzania yaliyoonekana kwenye mitandao mingi zaidi ya nje. Umaarufu wa wasanii hawa hauwezi kuepukika na Diamond akiongoza msafara.
Mtandao maarufu wa MSN ambao ndio dada wa anuani maarufu duniani ya hotmail jana imeandika habari picha iliyopewa jina la ‘The King and Queen of Bongo Flava’ na kuwataja Diamond na Lady Jaydee kama vinara nchini Tanzania.
“Bongo Flava is a genre of hip hop from Tanzania. The lyrics are in English or Swahili. Two of the biggest stars of this genre are Diamond Platnumz and Lady Jaydee,”umeandika mtandao huo kwenye page maalum kuhusu mambo ya Afrika ya ‘http://african.howzit.msn.com’ ambayo ni sehemu ya MSN inayoandaliwa nchini Afrika Kusini.
Kutokana na shavu hilo Diamond ameandika kupitia website yake, “Honestly nimejiskia furaha sana kuandikwa katika mtandao mkubwa kama huu,juu ya kazi yangu ya muziki ninayoifanya na kupewa heshima ya kuwa King of Bongo Flava.Hii inaonesha ni jinsi gani muziki wetu umepiga hatua na unazidi kuvuka boda.”
Big up Diamond na Lady Jaydee
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....