
MZEE huyu wa jamii ya kabila la wamasai 
aliyetambulika kwa jina la ''Tulito'' Mkazi wa KIA njia panda ya 
kuelekea uwanja wa ndege wa Kilimanjaro International Airpot, amepata ajali mbaya ya kugongwa
 na fuso alipofanya jaribio la kuvuka barabara hiyo ya lami ambayo magari
 huenda mwendo kasi.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka mkoni 
kilimanjaro 
kimedai
 kwamba gari hilo aina ya FUSO halikusimama baada ya kumgonja mzee 
Tulito, lilitokomea..! Raia waliokuwa karibu na eneo la tukio 
hawakufanikiwa kunasa hata namba za gari hilo, Mzee tulito 
aliwahishwa Hospitali wilayani boma kwa matibabu zaidi.
CHANZO : MATUKIO NA MICHAPO



0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....