Akizungumza wikiendi iliyopita katika Viwanja vya TCC
Chang’ombe jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na mechi kati ya wasanii
wa Bongo Fleva na Bongo Muvi, Ray aliwashangaa waandishi kwa
kumshambulia kutoka kimapenzi na Chuchu.
Mwandishi
alianza kwa kumwuliza: “Ray magazeti yanaandika kuhusu wewe kutoka na
Chuchu Hans ambaye ni mke wa mtu. Mainda amezungumza mengi. Kukaa kwako
kimya bila kufafanua chochote siyo kitu kizuri. Tafadhali, hebu zungumza
japo kidogo kuhusu madai ya Mainda.”
RAY: Sikia nikuambie, huyo Mainda utoto unamsumbua. Haniumizi kichwa kabisa. Kuhusu Chuchu... si mmeshaandika? Endeleeni kuandika lakini soon mtashuhudia kitu kikubwa sana.
RISASI: Ni kitu gani hicho?
RAY: Niacheni na Chuchu wangu.... kifupi ndiye mke wangu na itawashangaza wengi. Halafu mimi nawashangaa sana. Yaani mimi kutoka na Chuchu mnakuzaaaa... mbona alivyokuwa na ma-boyfriend zake wengine hamkuandika? Kwa sababu ni Ray basi mkaona ni habari. Mimi ninavyojua Chuchu siyo mke wa mtu.
Kwanza mimi sijamchukua kutoka mikononi mwa mumewe kama mnavyosema. Chuchu tayari alikuwa na maisha yake mapya. Nilimchukua kutoka kwa Libert (hajafafanua zaidi ni nani). Mbona alivyokuwa na huyo Libert hamkuandika? Kifupi niacheni na maisha yangu.
RISASI: Vipi kuhusu Johari?
RAY: (Huku akikimbia kuingia uwanjani) Tena huyo mama yako (akimuonesha mwandishi Johari) anakuja.
Mwandishi wetu aliachana na Ray aliyekuwa akiingia uwanjani na kumfuata Johari lakini hakuwa tayari kusema chochote achilia mbali hata kumsikiliza mwandishi wetu!
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni gazeti hili liliandika habari yenye kichwa MAINDA: NIMETOA MIMBA YA RAY. Ndani yake Mainda alifunguka mengi ikiwemo kuchanganywa kimapenzi na Ray, yeye na wenzake Johari na Chuchu Hans.

CREDIT:GPL
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....