"MGOGORO ULIOPO NDANI YA CHADEMA NI KAZI YA MAKACHERO..." DR SLAA AFUNGUKA

.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa amesema mgogoro uliopo ndani ya chama ni kazi ya makachero. Alitoa kauli hiyo jana jioni alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Kahama mara baada ya kuwasili akitokea jijini Dar es Salaam akiwa njia kuelekea mkoani Kigoma kwa ziara ya wiki moja.
 

Dk. Slaa ambaye alifika saa 12 jioni alitumia muda dakika zisizozidi 20 kuhutubia ambapo alisema chama hicho kina taarifa za ushiriki wa makachero, lengo likiwa kukidhoofisha na hatimaye kukisambaratisha chama hicho.

“Tunazo tayari taarifa kuwa makachero ndio wapo nyuma ya mgogoro ndani ya chama, wameingia kwa nia ya kutuvuruga, lakini tupo imara.

“Nawasihi Watanzania waache kushabikia vitu visivyo vya msingi, badala watumie muda wao kufikiri na kufanya mambo ya msingi kwa Taifa.

“Yote yanayotokea katika chama chetu kwa sasa yanatuandaa na kutukomaza kwa ajiri ya kuchukua madaraka ya nchi mwaka 2015,” alisema.

Alisema kuwa, wanachama wote wa Chadema wanapaswa kujua hakuna aliye juu ya Katiba ya chama hicho, kwa hiyo Katiba italindwa na kusimamiwa bila woga kwa maslahi mapana ya chama.

Leo anatarajiwa kuondoka na msafara wake kuelekea mkoani Kigoma, ambako kituo chake cha kwanza kitakuwa eneo la Kakonko na baadae ataelekea Muhambwe.

Katika ziara hiyo ya kukagua uhai wa chama atatembelea mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

1 comments:

  1. chadema isitafute mchawi mchawi wao wenyewe.. REST IN PEACE CHADEMA

    ReplyDelete

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter