Msanii wa Bongo Flava na producer/mmiliki wa studio ya 4.12, Dully Sykes amefunguka kwa kusema kama asingekuwa mwanamuziki ana mtayarishaji wa muziki basi leo hii angekuwa Houseboy.
Akizungumza na mwandishi wetu leo, Dully alisema anapenda kazi za upishi kutoka moyoni na kama asingekuwa hafanyi muziki basi angekuwa habanduki jikoni.
“Muziki umefanya watu wakose chakula kitamu,nilikuwa napenda kupika sana na bila kufanya kazi ya muziki na producer basi ningekuwa mpishi,” Dully.
Katika hatua nyingine, Dully amesema hivi karibuni ataachia ngoma yake mpya iitwayo, Kabinti Special.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....