Rapper Nay Wa Mitego amesema amekuwa akisumbuliwa mno na maafisa usalama pamoja na vyombo mbalimbali vya habari wanaomdhania kuwa anajihusisha na biashara ya madaya ya kulevya kitu ambacho amekuwa akikanusha kwamba sio kweli.
Akiongea na Bongo leo kwa njia simu Nay amesema anasikitishwa kupokea taarifa zinazodai kuwa anajihusisha na biashara hiyo haramu, kitu ambacho hakifanyi kwakuwa anategemea shughuli zake za muziki zinazomlipa vizuri.
“Watu wamekuwa wakishangaa sifanyi show hata mwaka mzima lakini maisha yanaenda namiliki gari ndio maana wanaongea mengi huku media na maafisa usalama wananichunguza kila siku,” alisema Nay.
Msanii huyo wa Salam Zao amesema yupo kwenye maongezi na kampuni ya simu ili imfanye kama balozi wake.
“Nasubiria mambo yangu yaende poa, nimeingia mkataba wa kuwa balozi wa mtandao wa simu hapa nchini bado muda wake kuuweka wazi kwasababu tupo kwenye makubaliano zaidi na pia ikifika muda nataka kuanika vyanzo vyangu vyote vya mapato, ” alisema.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....