PICHA za chumbani za mwigizaji Rose Ndauka na mchumba wake, Malick Bandawe zimevuja baada ya rafiki wa karibu wa wapenzi hao kuzisambaza kitaani.
Rafiki huyo wa karibu alizungumza na Weekly Star Exclusive na kusema kuwa wapendanao hao walikuwa wakilala katika hoteli moja iliyopo maeneo ya Mbezi Beach, jijini Dar kwa ajili ya kuilea mimba aliyonayo bibie.
“Huwa wanalala kwenye hoteli tangu mimba ilipoanza kuonekana, kusema kweli Malick anamlea Rose kama yai wasiwasi wangu atamlemaza wakati mjamzito anatakiwa afanye mazoezi,” alisema rafiki huyo kwa sharti la kutochorwa gazetini.
Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, Weekly Star Exclusive ilimuendea hewani Malick na kumuuliza juu ya picha hizo na suala la kuhamisha maskani hotelini hapo kama ni la kudumu au la! Alitiririka:
“Ni kweli nyumbani tunaenda mara mojamoja kwa sababu nahitaji mchumba wangu asiwe na msongo wowote wa mawazo, anahitaji sehemu ambayo imetulia ili ujauzito nao utulizane, muda mwingi tunautumia hotelini zaidi,” alisema Malick.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....