GIRLFRIEND AMLAZIMISHA BOYFRIEND WAKE APIGE MAGOTI HUKU AKIMCHAPA MAKOFI HADHARANI KWA KUMSALITI....


Unajua kama kitu hicho kingetokea hapa Africa,watu wengi wangesema kala 'majani' ni msemo unaotumika kwa mwanaume anayetawaliwa na mwanamke wake.

Seriously,mwanaume gani anayeweza kumruhusu girlfriend wake,mchumba au mke wake amdhalilishe hadharani namna hiyo?

Mwanamke mmoja wa kichina amekamatwa na polisi baada ya kumlazimisha boyfriend wake apige magoti huku akimpiga makofi usoni.

Udhalilishaji huu ulitokea ijumaa iliyopita kwenye mji wa Kowloon,Hong Kong baada ya Chui(boyfriend) kumchukua msichana mwingine na kumpeleka nyumbani kwake wakati  anamahusiano na Cheng(mpiga makofi).


Cheng alijua na akampigisha magoti boyfriend wake huyo mbele za watu wakipita.
Aliposisitiza kuwa hakumuita yule msichana kwake akisema 'sikiliza kwanza kabla hujanipiga',Cheng akaanza kumchapa makofi usoni huku anapiga kelele
 'You're slandering me!'




Watu wakajaa na kuanza kufilm tukio hilo la aina yake ambapo lilitumwa siku hiyohiyo YouTube.Watu wengine walipoanza kuingilia ugomvi huo wa kimapenzi Cheng akapayuka 'Haiwahusu!'
Watu wengi walioshuhudia walikuwa upande wa Chui,mwanamke mmoja akamwambia 'simama achana na mwanamke huyu mwenye sura mbaya,unastahili mzuri zaidi'
Mpita njia mmoja akawapigia simu polisi ambapo Cheng alikamatwa.
Mwanamke huyo mwenye miaka 20(Cheng)alikamatwa kwa kesi ya udhalilishaji wakati boyfriend wake mwenye miaka 23,Chui akipelekwa hospitali

Source:latestnews

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter