Mchakato wa kupiga kura ulianza mapema jana ambapo Makadinali 115 kutoka nchi 48 walikutana kwa faragha ili kumchagua atakaechukua nafasi ya aliyekuwa papa Benedikt wa 16 aliejiuzulu mwishoni mwa mwezi uliopita.
Zoezi la kupiga kura litaendelea hadi hapo mmoja wa Makadinali atakapopigiwa theluthi mbili ya kura yaani kura 77.
Atakaefikia kiwango hicho atakuwa Baba Mtakatifu wa 266.
Ikiwa Makadinali, wanaopiga kura watakubaliana juu ya Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki, moshi mweupe utatoka dohani na kengele zitapigwa kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....