Alfajiri ya leo, mtangazaji wa ITV anayejulikana kwa jina la Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na mchumba wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua.
Akizungumza na mnyetishaji wetu, kamanda Wambura ambaye ni kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Kamanda wambura amedai kuwa mwanaume aliyetenda mauaji hayo ni mchumba wake na alikuwa anafanya kazi katika umoja wa mataifa ( UN ) huko sudani ila bado haijafahamika kitengo alichokuwa akifanyia kazi.
Kwa mujibu wa Kamanda Wambura, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) ili awasuluhishe
Baada ya usuluhishi kuanza na kuonekana kuwa tatizo liko kwa mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa na mazoea ya kumtetea mwanae na ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro risasi ya kichwa na kumuua papo hapo....
Alipomuua mama huyo, mwanaume huyo alimpiga Ufoo Saro risasi mbili , moja ya tumboni na nyingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....