October
31 2013 kulikua na mechi ya Simba vs Kagera Sugar kwenye uwanja wa taifa
ambapo timu hizo zilitoka 1-1 huku goli lililoleta malalamiko likiwa ni
la Kagera Sugar ambalo lilifungwa kwa njia ya penat.
Kocha wa Kagera Sugar amesifia maamuzi ya refa na kusema
‘nafurahi timu imesawazisha kwenye dakika za mwisho na refa amefanya
kazi yake kwa
sababu ni siku nyingi sana marefa hawagawi penat kama hizo, timu nzuri
inacheza mpaka goli’
Kocha Kibaden wa Simba kasema ‘nashukuru tumemaliza
mpira salama na vijana wametoka salama, sijafurahishwa na jinsi mpira
ulivyochezeshwa, sitaki kusema hayo kwa sababu watu wana macho na
wanaweza kukosoa lakini
uamuzi haukuwa sawasawa, kama tutaendelea na mpira wa aina hii nafikiri
tutaondoka kwenye mwelekeo…
naomba TFF mpya iliyokuja ijaribu kutazama watu wapumbavu wa
aina hii wanaokuja pale kuwaudhi watu, sijafurahishwa na mpira
ulivyochezeshwa mwanzo hadi mwisho na nilijua kitatokea nini’
'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....