MUONEKANO mpya wa ‘kubugia kijusi’ wa msanii wa filamu za Kibongo, Rose Donatus Anjelus Ndauka ‘mtata’ umezua miguno, minong’ono huku ikionekana kivutio kwa wengi na kubaki wakihoji maswali yasiyojibika haraka, Risasi Jumamosi linaifunua.
Hayo yalichukua nafasi hivi karibuni wakati staa huyo alipofanya sherehe ya kutimiza miaka kadhaa tangu ‘anuse hewa ya Oksijeni’ iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Club Escape Beach Kigamboni jijini Dar na kuacha historia ya aina yake.
“Mh! hivi kweli Rose ana mimba?, siamini kama ameamua kuzaa kabla ya ndoa si alikuwa akikataa huyu? Sasa imekuwaje” alisikika mama mmoja katika sherehe hiyo.
“Ila kapendeza jamani, sasa kaonekana mwanamke kweli, muone anavyotembea kwa madaha, mimba hiyo imemuongezea mvuto!” alisema msanii mwingine wa kike mwenye ‘taito’ kubwa bongo.
Mwandishi wetu alipomuuliza Rose juu ya minong’ono hiyo, alijibu kwa kifupi huku akionekana kufurahia.
“Jamani sina jibu la kuwapa, kama watu wanashangaa ni wao niseme nini tena?” alisema Rose na kisha kufunga ‘faili’ la mazungumzo na mwandishi wetu
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....