Bomu hilo lilirushwa na watu wasiojulikana majira ya saa nne za asubuhi ambapo kanisa hilo lilikuwa linazinduliwa na a balozi wa Vatikan nchini, Fransisko Padika
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea asubuhi wakati balozi huyo akijiandaa kukata utepe wa kanisa hilo jipya
Sabas alisema kuwa wakati balozi huyo anakata utepe huo ghafla mtu asiojulika alirushwa bomu ambalo liliweza kuwajerui watu huku likisababisha mauti ya mtoto mmoja
“huyu balozi alikuwa hapa Arusha toka siku ya alhamisi lakini leo sisi tulikuwa na ulinzi wa kutosha juu yake lakini wakati anakata utepe ghafla alilipukiwa na bomu hali ambayo ilisababisha vurugu kubwa sana katika kanisa hilo jipya”alisema Sabasi
Pia aliongeza kuwa mpaka sasa polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye hajajulikana makazi yake lakini uchunguzi unaendelea huku jeshi hilo likiomba msaada wa wananchi lakini pia msaada wa majeshi mengine ili kuweza kuchunguza tatizo hilo.
wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiongea kwa niaba ya Serikali alisema kuwa wananchi wa jiji la Arusha hawapaswi kujiuliza chanzo na kuhusisha tukio hilo na imani za kidini bali wanatakiwa kutoa ushirikiano.
Alisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa majerui wote wanapata matibabu ingawaje bado kuna ukosefu wa vifaa katika hospitali ya mkoa wa Arusha (Mt Meru)
“kazi ya uchunguzi tunatakiwa kuachia vyombo vya usalama pekee tuwe watulivu na tutoe taarifa kwa Polisi lakini pia tunaomba msaada wa madaktari wa ziada katika hospitali kwani hawa majerui wameumia vibaya sana”alifafanua Magesa.
Wakati huohuo Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Goodbless Lema alisema kuwa matukio ya uharibifu wa makanisa ni mwendelezo wa kile kilichotokea Zanzibar, na Dar es Saalam lakiniSerikali bado haiskii wala kuona mpaka idadi kubwa sana ya watu wafe.
Lema alisema kuwa lazima mambo kama hayo yatatokea kwa kuwa wanasiasa wa sasa wanatafuta umaarufu kwenye makanisa hususani uzinduzi bila kujua na kutambua kuwa kuna hatari kama hiyo.
Aliyataka makanisa kuachana na tabia ya kuwa karibu na wanasiasa na badala yake wahakikishe kuwa wanajitegemea kwa michango yao wao wenyewe kwan kuwa siasa haziendi kabisa kwenye makanisa.
Hataivyo Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za mount Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi , wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina Fredirik, Joram kisera, Novelt John, Rose pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, .Wengine ni Lioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim.
Wakati huo huo jeshi la polisi limelazimika kutumia mabomu kumnusuru mwendesha boda boda mmoja katika eneo hilo anayedaiwa alimtorosha mtu anayesadikiwa alirusha bomu hilo lililoaangukia mbele ya kanisa hilo na kujeruhi waumini hao.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....