WASTARA AKATAA KUWA MKE WA PILI...!!!

http://api.ning.com/files/rCNzRKkcZYaRl8rT2Ghdp11G9XsjfHgOhCzL8GUhxCcWXmVRrcxNgzbihjqVgYMmwttiYFQiMBFUCChccEmDHRHxexbh7OqI/Wastara.jpg 
                                                      Wastara Juma.
MSANII wa filamu za Kibongo, Wastara Juma hivi karibuni alikataa kuolewa na kuwa mke wa pili baada ya kupigiwa simu na mwanamke mmoja jijini Dar akimtaka awe mke mwenzake.
Wastara ambaye hivi sasa yuko Uarabuni kwa ajili ya mapumziko baada ya kufiwa na mumewe, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Januari mwaka huu, alikataa ofa hiyo na kusema kwamba kwa sasa hafikirii kabisa kuolewa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, mwanamke huyo aliamua kufanya hivyo baada ya kushauriana na mumewe kuhusu Wastara kuingia katika familia yao.
“Mwenyewe alisema alishauriana na mumewe na haoni tatizo Wastara kuwa mke mwenzake kwa sababu imani ya dini yao inaruhusu,” kilieleza chanzo hicho.

UTHIBITISHO NI HUU
Baada ya kuzinyaka habari hizo, kama kawaida yate  lilimnyanyulia mkonga mwanamke huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe, akathibitisha kumpigia Wastara.
“Lengo langu lilikuwa zuri tu, unajua dini yetu ya Kiislamu inaturuhusu kuolewa wanawake mpaka wanne hivyo niliona ni heri nikae na mwenzangu.
“Halikuwa suala la kukurupuka...tulizungumza na mume wangu na tulishajipanga kwenda kutoa mahari kwao.  Nimesikitika sana alivyokataa ila namtakia kila la heri katika maisha yake,”
alisema.

WASTARA SASA
“Ni kweli nilipigiwa simu na mwanamke wa huko nyumbani (Tanzania), nilimjibu kama ninavyokuambia wewe sasa hivi, kwamba sifikirii kuolewa kwa sasa,” alisema Wastara kwa njia simu alipopigiwa na mwandishi wetu.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter