Habari ndugu zangu
Naombeni ushauri wenu kuhusu tatizo la dada yangu wa tumbo moja ambalo sikuwahi kulihisi, kulidhani wala kulijua kwa zaidi ya miaka 20. Kifupi mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 23 ( Natimiza miaka 24 mwezi Juni mwaka huu ). Kwa sasa ninasoma mwaka wa mwisho katika chuo kikuu kimoja hapa nchini .
Kwetu tumezaliwa watatu dada zangu wawili, wa kwanza alizaliwa miaka ya sabini ( R.I.P ) na huyu wa pili ambaye ndie point of discussion, alizaliwa mwanzoni kabisa mwa miaka ya 1980.
Ngoja niende moja kwa moja kwenye point, siku ya jumamosi iliyopita ( tarehe 27 APRILI 2013 ) saa nne kamili za asubuhi nilienda kumtembelea dada yangu ( hana mume, mtoto wala sijawahi kusikia chochote kuhusu kuwa na rafiki wa kiume yaani boyfriend )...
Nilienda pale kwa ajili ya kupiga mzinga kidogo na nilipanga kurudi hosteli ambako ninaishi siku iliyokuwa inafuata yani jumapili.
Mida ya saa sita mchana, aliwasili mdada mmoja ambaye ninamjua kama rafiki wa karibu wa dada yangu, tulisalimia kisha dada akaja kumpokea mgeni wake kisha wakaelekea ukumbini, baadaye nikarudi zangu chumbani kwangu na kuendelea kucheza na laptop yangu.
Yalipita kama masaa mawili hivi mdada mwingine aliwasili nyumbani na kuingia moja kwa moja chumbani kwa dadangu .Sikujua kilichokuwa kinaendelea maana wakati huo nilikuwa chumbani, ila nilikuja kujua baadaye kwamba kuna mdada mwingine alikuja nyumbani pale .
Nilikuja kustushwa baadaye na kelele za ugomvi mkubwa sana, zikitoka chumbani kwa dada yangu ambako nilisikia kelele, na matusi mazito yakiporomoshwa, vilio na chupa zikivunjwa vunjwa hovyo, sikuwa na jinsi nikaamua kukimbilia upande kilipo chumba cha dada yangu kutoa msaada.
Kufika sikuamini kilicho tokea, nilimkuta dada yangu na yule dada mwingine ambaye nilikuwa namjua kama rafiki yake wakiwa kama walivyo zaliwa, wamelewa wanagombana na huyu mdada mwingine aliyekuja wakati mimi nimo ndani, huyu dada mwingine alikuwa anamshambulia yule dada aliyekuja mara ya kwanza na dada yangu alikuwa anajaribu kumzuia..
Kilicho nishangaza zaidi kuhusu dada yangu ni kwamba ana u*me ( tena mkubwa tu kama u*me wa mwanaume rijali, na umevalishwa kinga ), mwanzoni nilidhani labda amevaa midoli lakini haikuwa hivyo, nii u*me kabisa...
Nilicho kifanya ni kumtoa yule dada aliyekuja mwishoni hadi nje kisha nikarudi zangu chumbani kwangu....
Sikufanikiwa kuongea na dada yangu usiku huo hadi kesho yake lakini sikuongea chochote kuhusu kilicho tokea jana yake .Japokuwa aliniomba radhi kwa kilicho tokea lakini hatukuzungumzia kabisa kuhusu suala la yeye kuwa na jinsia mbili..
Kusema ukweli suala hili linanikosesha sana raha na sijui nini cha kufanya.Nimepanga kutoongea na yoyote wala sitawauliza wazazi wangu lakini picha hii nitakaa nayo kwa muda mrefu sana, simuoni tena dada yangu kama nilivyo kuwa naumona hapo zamani..
Naombeni ushauri wenu .
Majidai
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....