Huyu ndie mfanyabiashara aliyesababisha kifo cha Koplo Erikiza askari wa usalama barabarani jijini Dar katika msafara wa JK na leo amefikishwa mahakama ya Mwanzo Iringa kwa kujipatia mali kidanganyifu |
Magari ya ndugu waliofika kumwekea dhamana mahakamani hapo leo
Mtuhumiwa wa utapeli ambae anadaiwa kusababisha ajali katika msafara wa JK akijificha wakati akitoka mahakamani baada ya kudhaminiwa kwa kiasi cha TSh milioni 15
Huu ndio usafiri aliotumia kujificha wakati akiondoka mahakamani hapo
Askari polisi akimsindikiza mtuhumiwa huyo wa utapeli huku akiwa amejificha sura kukwepa kamera ,leo katika mahakama ya Mwanzo Bomani Iringa |
Bw Jackson Simbo Stivin
MFANYABIASHARA mkazi wa Mbeya ambae alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T.328 BML aina ya Land Lover Discovery na kusababisha kifo cha askari mwenye namba WP 2492 Coplo Elikiza Nnko wakati wa msafara wa Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam ,amefikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya Mwanzo Bomani mjini Iringa kwa tuhuma za kujipatia gari lenye thamani ya Tsh milioni 30 .
Mfanyabiashara huyo Jackson Simbo Stivin(45) alifikishwa mahakamani leo asubuhi akituhumiwa kujipatia gari aina ya fuso lenye thamani ya Tsh milioni 30 ambalo ni mali ya mfanyabiashara wa mkoani Iringa Venansia Sanga.

Akisoma shtaka hilo hakimu wa mahakamani hiyo ya Mwanzo Bomani Mheshimiwa Alois Masua alisema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 4 mwaka 2012 katika eneo la Miyomboni mjini Iringa .
Mheshimiwa Masua alisema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kutenda kosa hilo alitoweka na kujificha katika mikoa mbali mbali hapa nchini .
Hata hivyo alisema kuwa mlalamikaji katika shtaka hilo baada ya jitihada za kumtafuta kushindikana ndipo alipofika mahakamani Februari 15 mwaka huu kufungua kesi namba 61 /2013 kuhusiana na mtuhumiwa huyo.
Alisema kuwa kutokana na kufunguiliwa kwa kesi hiyo jeshi la polisi kwa kushirikiana na mlalamikaji waliendelea kumsaka mtuhumiwa huyo bila mafanikio na baada ya kutokea ajali iliyosababisha kifo cha askari huyo wa usalama barabarani jijini Dar es Salaam katika msafara wa Rais Kikwete ndipo mtuhumiwa huyo alipokamatwa baada ya picha yake kuonekana katika vyombo vya habari .
Mtuhumiwa huyo amekana shtaka hilo dhidi yake na mahakama kudai kuwa dhamana yake ipo wazi na kuwa mdhamini anapaswa kusaini hati ya dhamana ya yenye thamani ya Tsh. milioni 15 masharti ambayo yalitimizwa na wadhamini na mfanyabiashara huyo kutolewa kwa dhamana hadi Aprili 25 kesi hiyo itakapotajwa tena.
Wakati huo huo ndugu wa mfanyabiashara huyo walionyesha kuwazuia wanahabari kumpiga picha wala kuandika habari hiyo kwa madai kuwa ni habari ndogo ambayo jamii haipaswi kuijua na kumtaka mfanyabiashara huyo kujifungika sura yake na kuondoka na msafara wa magari mawili ya kifahari katika mahakamani hiyo.

0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....