SHILOLE: NIMEJIFUNZA MAMBO MENGI SAUZI

BAADA ya kupiga shoo pande za Afrika Kusini, mwanadafada anayekimbiza kwenye anga la muziki wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema amejifunza mambo mengi kupitia ziara hiyo.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akipiga stori na Stori 3 juzikati baada ya kurejea Bongo, Shilole alisema kwanza amejitambua na kupata mbinu mpya za kuhimili jukwaa hata kwa watu wasioelewa lugha unayoimba, mbinu mbalimbali za kujitangaza na ushirikiano.
“Nimejifunza mambo mengi, muziki una nguvu kubwa watu wanakuelewa kama una mbinu za kuwashawishi unapokuwa jukwaani, mashabiki wangu waendelee kunipa sapoti kwani mambo ndiyo kwanza yameanza,” alisema Shilole.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter