'ROMA ANA DHARAU SANA'.....MASHABIKI

KAMA tulivyoahidi wiki iliyopita, msanii Ibrahim Musa ‘Roma’ yupo hapa kwa ajili ya kujibu na kufafanua maswali mliyomuuliza, shuka nayo.

Roma nakukubali sana kwenye gemu hauogopi kuiambia ukweli serikali, ila uko juu kimuziki. Elisha, Dar, 0715182591
ROMA: Shukrani sana, Hip Hop ni ukweli na uhalisia na ukweli una tabia ya kushinda na hofu ni dhambi kubwa!

Ibrahim Musa ‘Roma’.
MPANGO WA KUIMBA MAPENZI
Nasikia unataka kutoa singo ya mapenzi, ni kweli? Mud Muzungu, Dar, 0655288044
ROMA: Hahahaha nitoe mara ngapi? Hata  hizi  ninazoimba mbona  ni mapenzi? Sema ni mapenzi  kwa nchi yangu na jamii!
ANATOKEA MKOA GANI?
Roma wewe ni noma kwenye fani, unatokea wilaya ipi ya mkoani kwetu na ni kabila gani? Je, ni kwa nini huimbi mapenzi kabisa? Juliana Jang’andu, Dar, 0712089824
ROMA: Natokea  Tanga, asante.
BIFU LAKE NA JOH MAKINI
Vipi Roma, nasikia una bifu na Joh Makini kwa nini? Riziki Minde, Dar, 0716000045
ROMA: Linahitajika darasa  kubwa kuwaelimisha watu wajue nini maana ya bifu, battle, dis, ku-hate na ku-challenge n.k, all in all  sipo na bifu na  John Simon!! We all good brazaz!
ANADHARAU MASHABIKI
Roma mwanzoni nilikukubali sana lakini siku hizi unatudharau sisi mashabiki wako. Nakumbuka siku moja ulichelewa kwenye shoo pale Coco Beach na ulipofika kwenye Bajaj ukaanza kuzungumza maneno machafu. Je, ndiyo tabia yako sasa hivi? Mashabiki wako Kinondoni, Dar, 0776262439
ROMA: Si kweli na haitatokea.
KWA NINI SERIKALI?
Kaka Roma kiukweli unajua kuimba ila kwa nini katika nyimbo zako unazungumzia sana serikali? Nahitaji kufahamu. Maimartha, Dar, 0718445222
ROMA: Asante kwa kunipongeza, mimi nadhani serikali ndiyo muhimili mkuu wa nchi na vilivyomo ndani ya nchi, kwa hiyo chochote  utakachozungumzia lazima kihusiane na serikali, nyumba, mitaa, vijiji kila sehemu kuna serikali, hata ndani ya familia yako ipo serikali.
ANAFANYA NINI MBALI NA MUZIKI?
Mbali na muziki unajishughulisha na nini?  Rita, Dar, 0716752124
ROMA: Kwa sasa  naungana na wajasiriamali wote nchini katika kazi mbalimbali za uzalishaji mali wa taifa hili.
CHUO VIPI?
Vipi kuhusu chuo maana kuna kipindi nilikuwa nasikia upo chuo kwa hiyo umemaliza au? Ebahath, 0652011773
ROMA: Ndiyo nilikuwa pale UDSM, nimemaliza mwaka juzi 2011 nafikiria kuendelea na levo nyingine.
KUHUSU MGOGORO WA RUGE NA SUGU
Roma ni kweli fedha imemaliza mgogoro wa Ruge na Sugu au ni wimbo tu maana tumeona Sugu analalamika. Elia, Iringa, 0718085308
ROMA: Muziki ni sanaa  na  katika sanaa kuna fasihi, na  hii huwa  na mapokeo tofauti mbele ya  hadhira, ndiyo maana ukimuuliza Mpoto alipoimba mjomba alimaanisha nini? Atakujibu ni kaka yake mama ila wewe ulitafsiri vingine.
ANA MTOTO USANGARA?
Dah Roma nakukubali sana kwenye gemu unakimbiza lakini mbona tunasikia una mtoto mmoja usagara kaka tupe ukweli. Godbles Kweka, Arusha, 0714279798
ROMA: Asante kaka, ila wewe upo Arusha ya Tanga umeyajuaje? hahaha mtoto demu au mtoto wa kumzaa? Maana siku hizi hata  mama’ko unaweza kumwambia niaje mwanangu? Niaje mwana?

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter