Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar, jirani na nyumba ya staa mwenzake, Wema Sepetu ambapo Wolper aliyekuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota-Brevis Saloon alivaana uso kwa uso na gari lingine aina ya Toyota-Nadia.
Kwenye ajali hiyo, gari la Wolper lilibondeka mbele na kuvunjika kioo cha pembeni (side mirror).
Akizungumza na mwandishi wetu, Wolper alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kumshukuru Mungu kwa kumnusuru kwani hakuumia popote.
“Nilikuwa na mdogo wangu tunaelekea gereji kufuata gari langu, hili nililopata nalo ajali, siyo la kwangu hata sijui itakuwaje!” alisema Wolper.
Wakati huohuo, Hartman Mbilinyi ambaye ni prodyuza wa filamu, Jumatatu usiku alipata ajali baada ya gari lake kugongana na pikipiki wakati akirudi nyumbani kwake, Tegeta.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....