Kutokana na matokeo yaliotangazwa leo na tume ya uchaguzi ya kumpa ushindi Uhuru Kenyatta aliwashukuru wapiga kura kwa kujitokeza kwa wingi na aliishutumu tume kwa kushindwa kufanya maamuzi ya haki na kufanya madudu katika kuhesabu kura.
Aliendelea kusema serikali imetumia mamilioni kununua vifaa vya kisasa vya kuandikisha na kuhesabia kura lakini cha ajabu vifaa vilishindwa kufanya kazi na kusababisha kura kuhesabiwa upya kitu kilichofanywa kwa makusudi ili kupanga matokeo. Kamwe mimi na wafauasi wangu hatukubaliani na matokea na ili haki itendeke tutaelekea mahakamani na alimalizia kwa kusema mvumilivu ula mbivu kwa hiyo ndugu zangu tuvumilie tusubili maamuzi ya mahakama, asante kwa kunisikiliza.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....