ABIRIA WA PIKIPIKI AMTWANGA RISASI DEREVA WA DALADALA

NI huzuni kubwa ndani ya familia ya mzee Athumani Gogo, mkazi wa Chalinze, Pwani, kwa kifo cha mtoto wao mpendwa, Maneno Athumani aliyeuawa kwa kupigwa risasi.

Habari zinasema, Maneno, 22, aliuawa kwa bastola na mtu aliyekuwa amepakiwa kwenye pikipiki maarufu kama bodaboda na marehemu alikuwa akiendesha basi la daladala ambapo alipofika Sinza Kijiweni, aliuawa.
“Dereva aliyeuawa aliambiwa na watu hao kuwa ameziba barabara naye akawajibu kuwa mbona barabara ni kubwa, ndipo alipoambiwa na wauaji kuwa atakufa kifo kibaya,” alisema shuhuda aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
 Aliongeza kuwa dereva wa basi alipofika maeneo ya Sinza Kumekucha wauaji walisimamisha pikipiki yao mbele ya basi lake na abiria aliyekuwa amekaa nyuma ya mwendesha pikipiki alichomoa bastola na kumpiga risasi Maneno, hali iliyosababisha basi kuyumba na kutumbukia mtaroni.
Alisema baada ya wauaji kufanya hivyo walitokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP Charles Kenyela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na akafafanua kuwa wauaji bado wanasakwa.
“Tunawasaka waliofanya unyama huu na tutawapata, nawaomba raia wema watoe ushirikiano,” alisema Kenyela.


Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter