"VUMILIA MWENZANGU….NI IMANI YANGU KUWA KAJALA ATAACHIWA HURU"….MAMA LULU AKIMFARIJI MAMA KAJALA



BAADA ya mwanaye kutoka mahabusu kwa dhamana, mama wa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila, hivi karibuni alinaswa akimpa mbinu mama wa msanii Kajala Masanja zitakazomsaidia kumuokoa mwanaye.

Mama Lulu kushoto akiwa na mama mzazi wa Kajala (kulia).
Akina mama hao walinaswa na paparazi wetu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Kajala na mumewe, Faraja Chambo walifikishwa kwa ajili ya kujitetea kwenye kesi inayowakabili ya kutakatisha fedha haramu.
Kajala Masanja.
Katika tukio hilo, mama Lulu ndiye aliyeanza kufika mahakamani hapo na baada ya muda, alitokea mama Kajala ambapo walisimama chobingo na watu waliokuwa karibu yao walidai mama Lulu alikuwa akimpa mwenzake mbinu za kumwezesha kumuokoa mwanaye na kesi hiyo.
“Naona mama Lulu anampa mwenzake mbinu za kumuokoa Kajala ila amefanya la maana sana kuja kumpa kampani na kwa uzoefu wake wa mahakamani anaweza kumsaidia,” alidai mama mmoja aliyekuwa karibu yao.
Elizabeth Michael 'Lulu'.
Hata hivyo, wazazi hao walisitisha mazungumzo baada ya Kajala na mumewe kutolewa chumba cha mahabusu na kupandishwa kizimbani ambapo Wakili wa Serikali, Renald Swai aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 12 (kesho) baada ya kupokea udhuru kutoka kwa hakimu aliyetakiwa kusikiliza kesi hiyo, Sundi Fimbo.
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mama Lulu aliendelea kuwa karibu na mama Kajala ila kilichowatawanyisha kilikuwa ni mwanga wa kamera ya paparazi wetu.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter