Mrembo Hafsa Sasya aliyepigwa
Habari za kina kutoka ndani ya jeshi la polisi katika Kituo cha Oysterbay, Kinondoni, jijini Dar, zilidai kuwa Jack anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo ya Kinondoni, Dar kufuatia ule msala wa kumtwanga chupa nusu amuue mrembo aitwaye Hafsa Sasya.
Habari hizo zilieleza kuwa kilichokuwa kikisubiriwa ni kukamilika kwa upelelezi wa kipolisi baada ya pande zote kuhojiwa na uchunguzi kufanyika.
Ilifahamika kuwa kila kitu kimekamilika tayari kwa kesi hiyo kwenda mahakamani Jumatatu ya wiki ijayo.
Januari 26, mwaka huu, ndani ya Ukumbi wa Elements Lounge, Masaki, Dar, Jack alidaiwa kutofautiana na Hafsa ambapo alikwenda ‘toileti’ na aliporejea alikuwa na chupa aliyoitumia kumpasua usoni.
Katika tukio hilo, mwanadada huyo anayesifika kwa kuuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, alifikishwa polisi Oysterbay na kufunguliwa jalada la kesi namba OB/RB/1678/13-KUJERUHI.
Jack na Tiff walifunga ndoa mwaka juzi ambapo mwaka jana ilidaiwa kuvunjika baada ya mwanaume huyo kuwekwa nyuma ya nondo huku ikielezwa kuwa mkewe huyo hajawahi kwenda kumtembelea gerezani.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....