Wakizungumza na ‘kachala’ wa Funguka na Risasi hivi karibuni, jijini Dar kwa nyakati tofauti, wasanii hao kila mmoja alionekana kumtuhumu mwenzake kuwa ndiye kikwazo.
Flora Mvungi
Nini walichokisema na hatima ya ugomvi wao? Fuatana nami mstari kwa mstari.Funguka: Habari yako Flora, nimekupigia sana simu hupokei kwa nini?
Flora: Samahani nilikuwa ‘lokesheni’, nimerudi nikakuta ‘missed calls’ zako. Niambie una mpya? Maana wewe kupiga simu ni mpaka kuwe na jambo.
Funguka: Hujakosea, kikubwa nataka kujua hatima ya bifu lako na Shilole, limeisha?
Flora: Liishe wapi? Haliwezi kuisha mpaka aje aniombe msamaha. Yeye ndiye aliyelianzisha nikimwambia aje tuyamalize anakwepa, sijui ananitafuta nini huyu mwanamke.
Funguka: Inasemekana wewe na Flora mmewekeana bifu hilo kwa sababu ya kukuza majina yenu, ni kweli?
Flora: Siyo kweli, siwezi kufanya hivyo isitoshe jina langu ni kubwa katika sanaa. Hata kama ningetaka iwe hivyo, siwezi kufanya na Shilole kwani siyo saizi yangu na hana mvuto wa kufanya naye promosheni.
Funguka: Kwa nini mchumba wako Hamis Ramadhani ‘H.Baba’ asiwakutanishe na kulimaliza hilo bifu?
Flora: Haiwezekani kwani na yeye amemtukana hivyo siyo rahisi kutukutanisha.
Funguka: Ukiangalia chanzo cha ugomvi wenu ni nini hasa?
Flora: Swali hilo aulizwe Shilole kwani yeye ndiye aliyeanzisha.
Funguka: Sawa ngoja nimtafute.
Flora: Poa.
Funguka: Shilole habari yako.
Shilole: Salama kaka mzima?
Funguka: Mimi ni mzima, nimekutafuta ili kujua hatima ya bifu lako na Flora kwani wewe ndiye unadaiwa kumchafua mwenzako.
Shilole: Siwezi kukutana na Flora kwani nina mambo mengi ya kufanya na kinachonishangaza ni kwamba yeye anaenda kuongea na vyombo vya habari mambo yake ili ionekane mimi ndiyo namchafua. Siwezi kupoteza muda wangu kukaa kuongelea suala la msanii huyo kwani anasaka umaarufu kwa kutumia jina langu.
Funguka: Kwani wewe na Flora aliyetangulia kuwa na jina kubwa katika sanaa ni nani?
Shilole: Ni yeye, mimi nimekuja nyuma yake na nyota yangu ya sanaa imeng’aa na kumpita ndiyo maana sasa anahaha kusaka kurejesha jina lake kwa kutumia mgongo wangu. Mimi niko juu yake kwani Mungu amenifanikisha kufika hapa nilipo.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....