“Kwa kweli bunge letu linatia aibu kwa jinsi lilivyo hivi sasa limekuwa kama la wendawazimu na hii yote ni kwa sababu ya baadhi ya wabunge wanavuta bangi na kunywa pombe kabla ya kuingi bungeni, lazima hali hii ikomeshwe mara moja,” alisema Kigwangwala.
Hata hivyo, alipoulizwa majina ya wabunge hao wanaovuta bangi ni akina nani, alisema kuwa hawezi kuwataja kwani itakuwa ni uchochezi kwa kuwa kila mbunge anaingia bungeni kwa mamlaka aliyotumwa, wengine wameteuliwa na rais na wengine na wananchi na hakuna sheria inayowaadhibu.
Alipoulizwa kwa nini Spika, Anne Makinda anaacha baadhi ya wabunge waoneshe utovu wa nidhamu, alisema Makinda ana huruma tofauti na Spika aliyemtangulia Samweli Sitta ambaye alikuwa akitoa adhabu palepale kwa mujibu wa kanuni.
“Unajua kiti cha spika kina huruma sana kama kingekuwa kinatoa adhabu kwa kila mbunge anayevunja kanuni, basi bunge lisingekuws hivi, hata nikiwasilisha hoja binafsi kuhusu jambo hili itachukua muda mrefu kuwasilishwa, kilichobaki ni kuwashauri wabunge ili wajue kuwa bunge ni chombo kinachoheshimika,” alisema Kigwangwala.
Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Ezekiel Wenje alipoulizwa juu ya madai hayo ya wabunge kuvuta bangi na kunywa pombe kabla ya vikao alisema kuwa hana uhakika kama Kigwangwala ana ushaidi wa kutosha na hoja hiyo.
Naye, Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde akizungumzia sakata hilo alisema kuwa hakuna kitu kama hicho na wabunge wote wana nidhamu.
Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilillah alipotafutwa kwa simu juzi alisema mengi yamezungumzwa kuhusu jambo hilo na akamtaka mwandishi kufika ofisini kwake kupata maelezo zaidi.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....