WAKATI baadhi ya wasanii wakongwe kwenye tasnia ya filamu bongo wakionekana kupoteza umaarufu wao, msanii wa tasnia hiyo toka kitambo Johari, amedai kuwa inawezekana wasanii wakongwe wakawa wanapoteza majina yao lakini kwa ishu hiyo haiwafani wao washindwe kufanya kazi kwani bila wao tasnia ya filamu isingefika hapo ilipo sasa, ingawa kwa upande wake anaamini anaendelea kufanya poa.
Inawezekana ukawa unamtazama kwa macho ya kawaida msanii Johari, huku usijue kuwa yupo kwenye game toka kitambo tofauti na hawa unawaona sasa wanajizolea umaarufu pengine kuokana na tabia zao Johari ametoa mchango mkubwa hadi kusimamisha tasnia hii filamu huku akiaanzia kwenye maigizo ya kwenye TV.
Johari alisema kuwa wapo wasanii wengine wakongwe lakini hawaonekani wakifanya mambo ya ajabu ili waoenkana hovyo kwenye magazeti badala yake wanajikita kwenye kazi kwani wanajua wapi walikotoka si kama sasa kila mtu anafanya filamu bila kujua akina nani waliyoifikisha hapo ilipo sasa.
Alisema kuwa inawezekana wadau wa tasnia hiyo macho yao yakawa yanatazama wasanii wanaouza sura sana kwenye vyombo va habari hasa wale waliokuja juzi, lakini wao hawana shida na ishu hizo kwani umaarufu wao namna walivyokaa kwenye game wamejionea mambo mengine.
“Inawezekana wasanii wengine wakongwe wakawa wapo kimya na sio kwamba hawafanyi kazi bado wanaendelea kutoa filamu ingwa kuna mambo ambayo hawafanyi kama wanayofana wasanii waliokuja sasa kama kutafuta skendo na mambo mengi ya ajabu,” alisema.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....