JOHARI: SIJAWAHI KUWA NA RAY KIMAPENZI....USHAHIDI NINAO..!!




MSANII wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa, licha ya watu kudai kuwa yeye ana uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake Vincent Kigosi ‘Ray’, anaapa hawajawahi kufikia hatua hiyo.

Akizungumza na Amani hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar, Johari alisema amekuwa akikanusha madai hayo lakini anashangaa watu wanazikukomalia.

“Naapa sijawahi kulala na Ray. Nashangaa hizi habari zinavyozidi kuenea. Kwa hilo niko tayari kushika hata Biblia kuapia kuwa sina na wala sijawahi kuwa na uhusiano na Ray, uhusiano wetu ni wa kikazi tu,” alisema Johari.
Johari kwa muda mrefu amekuwa akidaiwa kutoka na Ray kwa siri lakini mwenyewe anakana huku wadau wakizidi kushikilia kuwa habari hizo zina ukweli ndani yake.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter