VITENDO mwa ukeketaji miongoni mwa jamii zetu zinaonekana kukoma lakini amini usiamini vitendo hivyo bado vinaendelea kushamiri huku vikionekana kufanywa na baadhi ya watu wachache ambao wamekuwwa wakivifanya vitendo hivi kwa siri kwa kuogopa kukamatwa na POLISI.
Mira hii potofu hapo mwanzo ilionekana kutapakaa maeneo mengihususani vijijini huku makabila kadhaa yakihusihwa na mila hizo potofu.
Litendo cha ukeketaji kwa wanawake ni kinyume kabisa na sheria inayomlinda mwanamke kwa sasa na yeyote anayehusishwa na vitendo hivyo basi hatua kali huchukuliwa dhidi yake.
Unayemwona kwenye PICHA ni mtoto mdogo wa kike ambaye alifanyiwa ukatili huo na watu wanaosadikiwa kuwa ni wazee wa kabila la KIMASAI ambao wameonekana kutojali sheria inayokataza vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu.
Mwandishi wetu ambaye alipata japo furs ya kukaa na watu hawa alijifunza mengi mazuri na mbaya pia kutoka kwa jamii ambayo imekuwa ikipigania mila yake kutoharibiwa na kitu chochote. Mwandishi ansema kitendo alichofanyiwa mtoto huyo kilikuwa ni cha Kinyama sana na kama wewe ni binadamu ambaye umeumbwa na roho basi hauwezi kuthubutu kumwangalia binadamu mwenzio akifanyiwa kitendo kama kile.
Pammoja na serikali kuipinga vilivyo MILA hii potofu lakini makabila mengi hapa nchini yameonekana kutotii AMRI hiyo ya SERIKALI.
Vitendo kama hivi vya unyanyasaji wa kijinsia haviwezi kuvumilika kwa namna yoyote ila na waalifu watachukuliwa ahatua mara moja.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....