MWANANFUNZI ABAKWA, NA KUNYONGWA KWA GAUNI LAKE!!



Binti mmoja  mwenye umri wa miaka 12 amefanyiwa kitendo cha kinyama kwa  kubakwa na kisha kunyongwa kwa gauni alilokuwa amevaa na kutupwa katika pagala la nyumba na mwili wake kuokotwa akiwa  amefariki dunia ,maeneo ya makoko darajani  manispaa ya musoma .
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa mara kamishina msaidizi Absalom Mwakyoma amesema kuwa mnamo 30,oktoba ,2012  majira ya 12.00 maeneo ya  makoko darajani uligundulika  mwili wa binti mmoja jina linahifadhiwa  kwa muda  aliyekuwa anasoma  darasa la sita katika shule ya msingi  makoko akiwa ameuwawa.
Mwakyoma alisema kuwa Uchunguzi wa awali unaonyesha  alifanyiwa  kitendo cha kinyama cha kuingiliwa ( kubakwa)na kisha  kunyongwa kwa gauni  alilokuwa amelivaa na kutupwa  kwenye pango la nyumba inayoendelea kujengwa.
Kamanda alisema kuwa mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi  na daktari wa hospitali ya mkoa wa mara  na kukabidhiwa  kwa ndugu zake  kuendelea na mazishi.
Kwa mujibu wa taarifa za wazazi  wake ,marehemu alitoweka  nyumbani na kuanza kutafutwa tangu 28,oktoba 2012
‘’’wauaji hawa wakati mwingine  ndugu zetu ,rafiki zetu ,shangazi  zetu ,wajomba zetu ,kaka zetu  binamu zetu  jirani zetu ,je tuwafumbie macho hadi lini ,kama mwana polisi jamii saidia  wafahamike ,watu hao wabaya wapo tunaisha nao alisema mwakyoma.
Aidha kamanda alitoa wito kwa yeyote  mwenye taarifa  zitakazosaidia kuwapata  watu wabaya hao wawasiliane kwa simu 0715009930 au za mkuu wa upelelezi  mkoani mara kwa namba 0712865725 ambapo zawazi zitatolewa.
Wakati huo gari ya kampuni ya bunda express yenye namba T810BDW SCANIA  bus ikiwa inaendeshwa na ramadhani  karimu 43) msambaa mkazi wa mwanza  alimgonga  mtembea kwa miguu aitwaye kizwere ndege 47) ,mzanaki  mkulima na mkazi wa irimba na kufariki papo hapo oktoba 30 .
Kamanda alieza chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi .
Mwakyoma amewaomba madereva  kuwa waangalifu  wanapoendesha  magari  kwa kuzingatia  sheria  za usalama barabarani  ili kuepusha  ajali

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter