WEMA 'amnasa' DALLAS wa WOLPER

MATUKIO yaliyozua gumzo kubwa kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ iliyofanyika hivi karibuni ni pamoja na lile la msanii wa filamu, Wema Sepetu kumnasa aliyekuwa mchumba wa Jacqueline Wolper, Ramadhani Mtoro ‘Dallas’.
Mapaparazi wetu waliotinga kwenye sherehe hiyo, walishuhudia ukaribu wa wawili hao na hata ulipofika muda wa kupiga picha, Wema alimkumbatia Dallas kimahaba, hivyo kuacha maswali mengi.
Mbali na hayo, Dallas alionekana kujipendekeza kwa msanii huyo kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu kuhisi anaweza kujiweka kwake.
“Na hivi Dallas hayuko tena na Wolper, si atahamishia majeshi kwake,” alisikika akisema kijana mmoja aliyekuwa eneo la tukio na mwingine akadakia:
“Kweli kabisa, hata Diamond anamzingua sana Wema kwa hiyo usije ukashangaa kusikia Wema kahamia kwa Dallas ili kumkomoa Wolper, si unajua hawa mastaa wetu!”
Katika kujua kilicho nyuma ya pazia, mwandishi wetu alimvutia waya Wolper na kumueleza yale yanayoendelea kwenye sherehe hiyo ikiwa ni pamoja na ukaribu wa Wema na Dallas ambapo alisema kwa kifupi: “Mimi najua kila kinachoendelea hapo, wala siumii kichwa.”
Naye Wema alipoulizwa kama ameamua kuhamishia majeshi kwa Dallas alisema, ukaribu wake na jamaa huyo si wa kiivyo watu wanavyofikiria.
“Dallas ni shemeji yangu kwa Diamond na Wolper jamani,” alisema Wema.
Katika hatua nyingine, Wema ameandika waraka mzito uliosheheni matusi akiuelekeza kwa baadhi ya mastaa ambao amewaweka kwenye mabano.
Waraka huo wenye maneno ambayo baadhi hayawezi kuandikwa gazetini uliotundikwa kwenye mtandao wa BBM ‘akiwadis’ baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijifanya kumuita mama kumbe wana lao jambo.
Sehemu ya waraka huo unasomeka hivi:
Jamani nimechoka na unafiki wa ki…(tusi) wa watu kujipendekeza kwangu for a purpose. I am tired. Mimi siyo mjinga wenu au fala au chuma ulete wenu wa kuwagharamia maisha yenu for no good reason. 
Natangaza rasmi kwanza mimi sina mtoto coz hapa nilipo sijazaa so siitwi mama… I am plain Wema Sepetu mpaka pale nitakapoamua kuzaa (hii ni kwa wale waliozoea kuniita mama).
Unafiki wa ki…(tusi), kunichekea Kichina sitaki. So fanyeni yenu. Nikija kufilisika mtakuwa na mimi?
Dah!Kweli mjini shule ku….(tusi)….” 
Baada ya kusoma waraka huo, Ijumaa lilimtafuta Wema na kumuuliza sababu ya kuuandika ambapo alisema amechoka, hivyo ameamua kuwafungukia wanafiki wake.
“Ni kweli kabisa nilimuomba Mungu aniongoze kufanikisha kuandika waraka huo ambao umeuona, kwani nimegundua mambo mengi sana nyuma ya pazia, mtu anajifanya kukuita mama, unamsaidia kwa mambo mbalimbali kumbe ni mnafiki, sasa kwa taarifa yao nimeshituka wa…. (tusi) na bado huo ni mwanzo tu,”

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter